Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yamficha kocha mpya Dar

Muktasari:

  • Yanga inatafuta kocha mpya baada ya Miloudi Hamdi kumaliza mkataba wake na kuondoka ambapo ameshajiunga na Al Ismailia ya nchini Misri akiwa anaondoka kwenye timu hiyo baada ya kuipa makombe matatu kwa muda mfupi.

Kocha mpya wa Yanga tayari ameshatua hapa nchini kuanzia wiki iliyopita na anaishi kwenye hoteli moja ya kifahari jijini Dar es Salaam.

Yanga imemaliza msimu uliopita na pointi 82, ikishinda mechi 27, sare moja na kupoteza miwili kati ya 30 iliyocheza, ikitwaa taji la 31, la Ligi Kuu tangu mwaka 1965, huku likiwa ni la nne mfululizo kuanzia msimu wa 2021-2022, 2022-2023, 2023-2024 na 2024-2025, lakini pia ikitwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB, Kombe la Toyota, Kombe la Muungano na Ngao ya Jamii.

Yanga inatafuta kocha mpya baada ya Miloudi Hamdi kumaliza mkataba wake na kuondoka ambapo ameshajiunga na Al Ismailia ya nchini Misri akiwa anaondoka kwenye timu hiyo baada ya kuipa makombe matatu kwa muda mfupi.

Timu hiyo yenye maskani yake Jangwani inatarajia kuanza maandalizi ya msimu mpya wiki ya mwisho ya mwezi huu na katika maandalizi yao itacheza mechi na timu kubwa inayoshiriki Ligi Kuu ya England.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha ndani cha uhakika kimesema kuwa kocha huyo aliwasili tangu wiki iliyopita na tayari ameshamalizana na Yanga, kinachosubiriwa ni kutangazwa hadharani siku chache zijazo.

"Kocha ameshatua nchini tangu wiki iliyopita na ameshamalizana na Yanga kila kitu kilichobaki ni utaratibu wa klabu tu kumtangaza.

"Bado yupo hotelini amekutana na uongozi tu hakuna hata mchezaji ambaye amewasiliana naye, lakini anatumia muda mrefu kukitazama kikosi na uhakika ni kwamba atashauriana na uongozi kuhusu usajili mpya na tayari kuna kazi imeshaanza kufanyika," kilisema chanzo.

Hata hivyo pamoja na kwamba chanzo hakikumtaja, lakini kuna asilimia kubwa sana kuwa kocha huyo ni Mfaransa Julien Chevalier aliyemaliza mkataba na kikosi cha ASEC Mimosas ya Ivory Coast na amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa anaweza kujiunga na timu hiyo ya Jangwani.

Mbali na kuifundisha ASEC kocha huyo mwenye miaka 44 pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Togo, akiwa amekaa ASEC tangu mwaka 2019.

Kocha huyo atakuwa na mtihani mzito kwenye kikosi hicho baada ya kuelezwa kuwa amepewa tageti ya kuhakikisha anachukua makombe yote ya ndani msimu ujao pamoja na kufika mbali kwenye michuano ya Ligi  ya Mabingwa Afrika ambayo Yanga itashiriki msimu ujao.

"Klabu imempa malengo kama ambavyo wamekuwa wakipewa makocha wengine wanaotua Yanga, lakini kubwa ni kuhakikisha anachukua makombe yote ya ndani msimu ujao, hii ndiyo tageti ya Yanga kila msimu, lakini kwake anatakiwa kufanya vyema kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, kuanzia kufika nusu fainali na kuendelea ni kocha anayefahamu sana soka la Afrika hivyo inaaminika kuwa anaweza kufanya kazi yake vizuri," kilisema chanzo hicho.


Aucho asaini

Yanga imefanikiwa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kiungo wake mahiri, Khalid Aucho.

Staa huyo raia wa Uganda amekuwa na mafanikio makubwa Yanga na kufanikiwa kutwaa makombe manne ya Ligi Kuu Bara.

"Aucho amesaini mkataba wa mwaka mmoja, ni mwanzo wa kazi ya kubakiza wachezaji wetu mahiri, naamini hadi timu inakwenda kwenye maandalizi ya msimu ambao nafikiri timu itaondoka Julai 22, wachezaji wote wanaotakiwa kusaini, watakuwa wameshafanya hivyo