Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wajasiriamali wawili wajishindia Sh857 milioni SportPesa

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa SportPesa Tanzania, simulizi za washindi hao zinaakisi mwenendo wa kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake katika michezo ya kubahatisha nchini, hususan kwenye michezo ya Aviator na Supa Jackpot.

Dar es Salaam. Wanawake wawili wajasiriamali kutoka maeneo tofauti nchini wameandika historia baada ya kujishindia jumla ya zaidi ya Sh857 milioni kupitia michezo ya kubahatisha ya SportPesa Tanzania, mafanikio yanayoonyesha kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake katika sekta hiyo.

Washindi hao ni Grace George Litimba na Husna Dauda Abubakari ambao kwa nyakati tofauti walifanikiwa kujishindia fedha hizo kupitia michezo ya Aviator na SportPesa Supa Jackpot.

Ushindi wao umeibua mjadala kuhusu ongezeko la ushiriki wa wanawake katika michezo ya kubahatisha, ambayo kwa muda mrefu ilionekana kutawaliwa zaidi na wanaume.

Grace aliandika historia baada ya kujishindia Sh400 milioni kupitia mchezo wa Aviator, na kuwa mshindi mkubwa zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Tanzania katika mchezo huo.

Ushindi huo ulimfanya kuwa miongoni mwa washindi wakubwa zaidi kuwahi kutokea katika majukwaa ya SportPesa Tanzania.

Grace, ambaye ni mwalimu, mfanyabiashara na mama mwenye umri wa zaidi ya miaka 50, amesema ushindi huo umebadilisha maisha yake na kumpa fursa mpya za kujiendeleza kiuchumi.

“Ushindi huu umebadilisha kabisa maisha yangu. Nataka kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya maisha yangu ya baadaye kwa kuongeza uwekezaji, kukuza biashara na kusaidia familia yangu,” amesema Grace.

Wakati simulizi ya Grace ikiendelea kuvutia wengi nchini, mwanamke mwingine, Husna Dauda Abubakari, aliibuka na ushindi mkubwa kupitia SportPesa Supa Jackpot. Husna, (36) ambaye ni mfanyabiashara kutoka Kibaha mkoani Pwani, alijishindia Sh457 milioni baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya mechi zote 14 zilizokuwa kwenye jackpot hiyo.

Husna, ambaye pia ni mama wa mtoto mwenye mwezi mmoja na shabiki wa klabu ya Yanga, alifika katika ofisi za SportPesa Tanzania kupokea ushindi wake akiwa ameambatana na mume wake pamoja na wanafamilia wengine.

Akizungumzia ushindi huo, Husna amesema mwanzoni alishindwa kuamini alichokiona baada ya matokeo kutoka rasmi.

“Nilipoona matokeo kwa mara ya kwanza sikuamini kabisa. Niliendelea kuyaangalia tena na tena kwa sababu kushinda kiasi hiki ilikuwa ni ndoto kwangu. Huu ni ushindi ambao umebadilisha maisha yangu na familia yangu kwa ujumla,” amesema Husna.

Amesema licha ya ushindi huo, alikuwa ameandaa pia mkeka mwingine wa jackpot ya mechi 16 uliokuwa na zawadi ya zaidi ya Sh800 milioni, lakini hakufanikiwa kuuweka kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha wakati huo.

Akizungumzia ushindi wa wanawake hao wawili, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa SportPesa Tanzania, Tracy Humplick, amesema simulizi zao zinaonyesha jinsi sekta ya michezo ya kubahatisha inavyoendelea kukua na kuvutia washiriki kutoka makundi mbalimbali ya jamii.

“Grace na Husna wanatoka katika vizazi tofauti na kila mmoja ana simulizi yake ya maisha. Hata hivyo, wote wameunganishwa na jambo moja, ambalo ni kushuhudia ushindi uliobadilisha maisha yao kupitia majukwaa yetu. Hii inaonyesha kuwa fursa za mafanikio zinaweza kumpata mtu yeyote bila kujali umri au mazingira yake,” amesema Tracy.

Kwa mujibu wa SportPesa Tanzania, simulizi za washindi hao zinaakisi mwenendo wa kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake katika michezo ya kubahatisha nchini, hususan kwenye michezo ya Aviator na Supa Jackpot. Kampuni hiyo inaeleza kuwa wanawake wengi zaidi sasa wanajitokeza kushiriki katika michezo hiyo, huku baadhi yao wakifanikiwa kupata ushindi mkubwa na kuvunja rekodi zilizokuwepo awali.