Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji: Tupo tayari kuivaa Morocco

Dar es Salaam. Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wamesema wapo tayari kwa ajili ya kulipambania taifa lao, wakiamini wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

Stars inacheza kesho saa 2:00 usiku dhidi ya Morocco, kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), michuano inafanyika nchini Ivory Coast.

Kipa wa timu hiyo, Beno Kakolanya amesema ingawa ni michuano migumu, lakini wapo tayari kwa ajili ya kuitetea bendera ya taifa, ili ipepee kwa heshima.

"Tumejiandaa, saikolojia zetu zipo vizuri, tunajua tunaliwakilisha taifa letu, kwa hiyo tutapambana kwa kadri tuwezavyo ili kupata ushindi,"amesema.

Kwa upande wa beki wa timu hiyo, Abdi Banda, amesema wamepata ujasiri wa kwenda kupambana zaidi baada ya kuona baadhi ya timu kubwa kusuluhu na zingine kupoteza mechi.

Banda ambaye anacheza soka la kulipwa Afrika Kusini amesema"Nilichokigundua kwenye michuano hii ni wachezaji tujitoa kwa asilimia mia kwa ajili ya taifa letu na sisi wenyewe.

"Ni michuano inayohitaji kutumia akili kubwa na nafasi, ila tunaweza kufanya vizuri,hakuna njia nyingine ya kutubeba zaidi ya kupambana kwa bidii."