Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uwanja wa Jamhuri wafungiwa, Simba yarejeshwa Chamazi

Muktasari:

  • Simba iliuchagua Uwanja wa Jamhuri na kufanikiwa kuchezea mchezo mmoja dhidi ya Tanzania Prisons ambapo ilikubali kichapo cha mabao 2-1.

Bodi ya Ligi Kuu Bara imeufungia Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Morogoro ikiwa siku chache baada ya Simba kuuchagua wake wa nyumbani na kuutumia kwa mchezo mmoja, badala yake imeirudisha timu hiyo katika Dimba la Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Simba iliuchagua Uwanja wa Jamhuri na kufanikiwa kuchezea mchezo mmoja dhidi ya Tanzania Prisons ambapo ilikubali kichapo cha mabao 2-1.

Siku chache baada ya mchezo huo Bodi ya Ligi imetangaza kusitiza kutumika kutokana na upungufu kadhaa kwenye miundombinu ya uwanja inayosaidia urushaji wa matangazo mubashara ya runinga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya habari na mawasiliano ya Bodi ya Ligi (TPLB), uamuzi huo umefanyika baada ya mdhamini mwenye haki za kurusha matangazo ya runinga, Azam Media, kulalamikia kuhusu changamoto walizokutana nazo katika maandalizi na urushwaji wa matangazo.

Taarifa hiyo imesema Simba ambayo ilichagua uwanja huo kwa mechi za nyumbani, ilishiriki kikamilifu katika majadiliano yaliyozaa uamuzi wa kusitisha matumizi ya Jamhuri na sasa itatumia Uwanja wa Azam Complex.

TPLB imesema Uwanja wa Jamhuri utatumika kwa michezo ya mashindano mengine yote yaliyo chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikiwemo Ligi ya Championship na First League yanayoendeshwa na kusimamiwa na Bodi ya Ligi.