Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upepo wa Southampton ulivyoibwaga Arsenal Kombe la FA

Muktasari:

  • Arsenal sasa imebaki katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Klabu ya Southampton imeandika historia baada ya kuifunga Arsenal mabao 2-1 na kutinga katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA.

Ushindi huo umeibua kumbukumbu za mwaka 1976, ambapo Southampton iliokuwa daraja la pili iliwashangaza wengi kwa kutwaa taji hilo baada ya kuifunga Manchester United fainali. Na sasa, miaka 50 baadaye, imeonekana kufuata nyayo hizo.

Kwa upande wa Arsenal, hili ni pigo jingine katika msimu wao ambao unaanza kuyumba. Hivi karibuni walinyang’anywa ubingwa wa Kombe la Carabao na Manchester City na sasa wameondolewa pia kwenye Kombe la FA, jambo linalotia shaka uwezo wao wa kuhimili ushindani wa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Bao la kwanza la Southampton lilitokana na kosa la beki wa Arsenal, Ben White, ambaye alikosea kupiga mpira wa juu na kumpa nafasi Ross Stewart ambaye alifunga kwa shuti kali.

Arsenal walijibu mapigo baada ya kusawazisha bao hilo kupitia mshambuliaji wao, Victory Gyokeres lakini juhudi zao hazikudumu kwa muda mrefu. Southampton waliendelea kushambulia kwa kasi na kuonyesha dhamira kubwa ya kushinda.

Katika dakika za mwisho za mchezo, kiungo Shea Charles aliibuka shujaa kwa kufunga bao la ushindi, na kupeleka furaha kubwa kwa mashabiki wa Southampton.

Arsenal sasa imebaki katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako nako ipo katika hatua ya robo fainali ikitarajia kuvaana dhidi ya Sporting CP wiki ijayo katika mchezo wa kwanza nchini Ureno kabla ya kurudiana jijini London, Aprili 15 mwaka huu.