Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yaichakaza Liverpool, Haaland akitamba

Muktasari:

  • Manchester City mwezi uliopita ilitwaa ubingwa wa Kombe la Carabao ikiichapa Arsenal mabao 2-0.

Manchester City imetinga nusu fainali ya Kombe la FA baada ya leo Jumamosi, Aprili 4, 2026 kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Liverpool nyumbani katika Uwanja wa Etihad.

Katika mchezo huo, Erling Haaland ameifungia Manchester City mabao matatu (hat trick) huku lingine moja likipachikwa na Antoine Semenyo.

Katika mchezo huo, Mohamed Salah ameinyima Liverpool angalau bao la kufutia machozi baada ya kukosa mkwaju wa penalti.

Ushindi huo umeifanya Manchester City kuandika rekodi ya kuwa timu ambayo imecheza mechi nyingi mfululizo za Kombe la FA nyumbani bila kupoteza.

Timu hiyo haijapoteza mechi 18 mfululizo za Kombe la FA katika Uwanja wake wa Etihad.

 Mara ya mwisho kwa Manchester City kupoteza mchezo wa Kombe la FA nyumbani ni miaka 11 iliyopita ambapo ilifungwa mabao 2-0 na Middlesbrough katika raundi ya nne ya mashindano hayo.

Katika hatua nyingine, matokeo hayo ya leo yameifanya Man City kumaliza unyonge wao dhidi ya Liverpool katika Kombe la FA ambapo kabla ya hapo, walikuwa wamepoteza mechi nne za nyuma za mashindano hayo dhidi ya Liverpool.

Ushindi huo wa Manchester City leo umeiweka timu hiyo katika uwezekano wa kumaliza msimu huu na mataji matatu mengine yakiwa ni Carabao ambalo tayari imeshalinyakua na lile la Ligi Kuu ya England kwani inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo nyuma ya Arsenal.

Kwa upande mwingine matokeo ya leo hapana shaka yameongeza presha kwa Meneja wa Liverpool, Arne Slot ambaye sasa anakabiliwa na mashinikizo ya kutimuliwa kutokana na timu hiyo kukabiliwa na msimu usio wa kuvutia.

Kutolewa katika Kombe la FA kumeifanya Liverpool ibaki na matumaini ya kutwaa taji moja tu msimu huu ambalo ni la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mabingwa hao wa taji la EPL msimu uliopita, katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu watakabiliana na PSG katika hatua ya robo fainali.