Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yapanda ubora viwango vya FIFA

Muktasari:

  • Tanzania ni miongoni mwa mataifa 24 ambayo timu zao za taifa zitashiriki katika Fainali za Mataifa ya Afrika ambazo zitafanyika Ivory Coast mwakani 2024.

Dar es Salaam. Tanzania imepanda kwa nafasi mbili katika viwango vya ubora wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwezi Septemba.

 Ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Niger na sare tasa ya ugenini dhidi ya Algeria katika mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2023 zitakazofanyika mwakani huko Ivory ni matokeo yaliyoonekana kuchangia kuibeba Tanzania katika viwango hivyo vya ubora vilivyotolewa jana, Septemba 21.

Kwa mujibu wa viwango hivyo vya ubora, Tanzania imepanda hadi nafasi ya 122 kutoka ile ya 124 ambayo ilikuwepo katika viwango vilivyopita vilivyotolewa Julai.

Licha ya kutofuzu Afcon, Uganda imepanda kwa nafasi tatu kutoka ile ya 92 iliyokuwepo awali hadi ya 89 huku ikiendelea kuongoza kwa upande wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Wakati Uganda na Tanzania zikipanda, mambo yamekuwa sio mauzi kwa Kenya ambayo imejikuta ikiporomoka kwa nafasi nne kutoka ile ya 105 iliyokuwepo Julai hadi nafasi ya 109 ingawa bado inashika nafasi ya pili kwa ukanda wa Cecafa nyuma ya Uganda.

Moroco iliyo katika nafasi ya 13 kidunia, inaongoza chati ya ubora kwa upande wa Bara la Afrika ikifuatiwa na Senegal iliyo nafasi ya 20 duniani, Tunisia walio nafasi 29 kwenye chati za Fifa wako nafasi ya tatu kwa Afrika huku nyuma yao wakiwepo Algeria na Msiri ambazo ziko nafasi ya 34 na 35 kidunia mtawalia.

Hakukuwa na mabadiliko yoyote katika chati ya nchi tano zinazoongoza kwa ubora duniani ambapo zile zilizokuwa katatika nafsi hizo bado zimeendelea kuwepo hapo.

Argentina imendelea kuongoza ikifuatiwa na Ufaransa, Brazil, England na Ubelgiji.