Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tabora United, Simba utam uko hapa

Muktasari:

  • Simba katika mechi 15 imekusanya pointi 40 na Tabora United katika mechi 16 imekusanya pointi 25.

Dar es Salaam. Mabenchi ya ufundi ya Simba na Tabora United yamesema kuwa timu zao ziko tayari kwa mechi ya kesho baina yao ambayo itachezwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora kuanzia saa 10:00 jioni.

Kocha wa Simba, Fadlu Davids amesema kuwa timu yake ipo tayari kwa mechi hiyo na atawakosa wachezaji wawili ambao ni Awesu Awesu na Aishi Manula

“Tunawaheshimu Tabora imekuwa ni tofauti na timu tuliyocheza nayo nyuma. Chini ya kocha mpya wamekuwa na mpangilio, wana wachezaji wazuri. Ni mechi tofauti wameimarika na sisi pia ni timu tofauti na tulivyokuwa mzunguko wa kwanza.

“Kama mechi yoyote tunayocheza, tunakuwa na maandalizi yanayofanana. Tutashambulia kwa njia tofauti. Kila mechi ni tofauti na eneo la kuchezea litaamua. Awesu hajasafiri na sisi na Aishi anasumbuliwa na mafua na tunasubiria ripoti ya daktari,” amesema Fadlu.

Kocha wa Tabora Kiazmak Anicet amesema kuwa amejiandaa kucheza na Simba na anatambua ubora wa wapinzani wake.

“Naamini wachezaji nilionao watafanya kazi na watajituma kwa ajili ya kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo huu. Nitapanga timu yangu kwa namna itakavyokuwa tayari kwa mchezo.

“Nimejitahidi kuweka timu yangu fiti na naamini wachezaji wangu watatumia vizuri nafasi watakazopata. Sitaki kuahidi kama tutashinda Iła tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” amesema Kiazmak.

Ushindi katika mechi ya kesho utaifanya Simba kufikisha pointi 43 na hivyo kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi wakati Tabora United kama itapata ushindi, itafikisha pointi 28 ambazo zitaifanya ijikite katika nafasi ya tano.

Katika mechi tatu zilizopita za Ligi Kuu baina ya timu hizo, Simba imeibuka mshindi mara zote.

Katika mchezo huo wa kesho, Tabora United hapana shaka itakuwa na hamu ya kulipa kisasi cha mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam, Agosti 18, mwaka jana ambayo Simba ilishinda mabao 3-0, yaliyofungwa na Che Malone Fondoh, Valentino Mashaka na Awesu Awesu.