Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs yagoma kushuka daraja

London, England. Kocha Mkuu wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi anaamini kwamba timu yake itapata ushindi katika mechi tano zilizobakia na kufanikiwa kubakia katika Ligi Kuu England (EPL).

Timu hiyo juzi usiku ilijikuta ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 nyumbani na Brighton licha ya kutangulia kufunga mara mbili, matokeo ambayo yameifanya ibakie katika nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi hiyo.

Na kama Spurs itamaliza katika nafasi hiyo, itakuwa miongoni mwa timu tatu zitakazoshuka daraja msimu huu.

Hata hivyo De Zerbi ambaye ameiongoza timu hiyo katika mechi mbili tangu alipojiunga nayo mwezi uliopita, anaamini Tottenham Hotspur inaweza kukusanya pointi 15 katika michezo iliyo mkononi na kubaki salama.

"Mara zote naamini katika ubora wa wachezaji. Walicheza mechi nzuri (dhidi ya Brighton). Nadhani tunaweza kucheza vizuri zaidi ya leo (juzi) kwa ubora zaidi, utulivu hasa tunapokuwa na umiliki wa mpira lakini kwa nyakati hii tunahitaji roho hii, mtazamo huu, fikra hii, na bado haijaisha.

"Tuna mechi nyingine tano. Ni ngumu, kila mmoja wetu anajua ni nyakati ngumu. Ni hali ngumu lakini tuna mechi nyingine tano, pointi 15 na timu hii ina uwezo wa kushinda mechi tano mfululizo," alisema De Zerbi.

De Zerbi amesema kuwa anaamini Spurs itawashangza wengi katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu kwa kusalia katika ligi.

"Sasa ni vigumu kusikia maneno yangu, lakini ukiwaangalia wachezaji, ukichambua kiwango chao, nafikiri tunaweza kushinda michezo mitano mfululizo.

“Sio kwa majivuno, kwa sababu mimi si mwenye majivuno, hasa kwa sasa, lakini tuna ubora wa kutosha kupambana na kushinda michezo mfululizo,” alisema De Zerbi.

Raia huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 46 ametoa msisitizo kuwa atamuondoa klabuni hapo mtu yeyote ambaye ana mtazamo hasi.

"Sina muda wa kuona watu wenye mtazamo hasi, kuona wachezaji wenye huzuni au wasaidizi wenye huzuni. Hapana.

“Tuna bahati kwa sababu tunafanya kazi katika klabu kubwa, uwanja mkubwa, tunacheza Ligi Kuu. Tuna sifa sahihi za kushinda mchezo, hivyo tunapaswa kuwa chanya, kwa sababu sipendi watu wanaolia, wanaofikiri kwa njia hasi,” amesema De Zerbi.


Mechi tano EPL zilizobakia Spurs

1. Wolves vs Spurs

2. Aston Villa vs Spurs

3. Spurs vs Leeds United

4. Chelsea vs Spurs

5. Spurs vs Everton