Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yafuzu robo fainali kwa sare Angola

Muktasari:

  • Simba inatinga robo fainali ya mashindano ya klabu Afrika kwa mara ya sita, nne ikiwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na mbili katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Sare ya bao 1-1 ambayo Simba imepata ugenini dhidi ya Onze Bravos ya Angola, imeihakikishia kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Bao la kusawazisha la Leonel Ateba katika dakika ya 69, limeifanya Simba ifikishe pointi 10 ambazo zimeendelea kuiweka katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi lake.

Simba imefuzu kwa vile Onze Bravos licha ya kwamba inaweza kufikia idadi ya pointi  zao 10, Simba itasonga mbele kwa kubebwa na kanuni ya kuwa na matokeo bora zaidi dhidi ya Onze Bravos.

Simba katika mchezo wa kwanza dhidi ya Onze Bravos uliochezwa Dar es Salaam, iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kufuzu kwa Simba kumechagizwa zaidi na ushindi wa mabao 3-0 ambao CS Constantine imeupata nyumbani dhidi ya CS Sfaxien.

Ushindi huo wa Constantine umeifanya ifikishe pointi 12 na kuongoza msimamo wa kundi A.

Bao la Ateba lilitokana na krosi iliyopigwa kutokea upande wa kulia na Shomary Kapombe akisawazisha bao la dakika ya 13 la Mosiatlhaga Abednego.

Safari ya Simba kuisaka hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu ilianza kwa ushindi nyumbani dhidi ya Bravos kisha ikafungwa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Constantine.

Baada ya hapo ikaibuka na ushindi wa mabao 2-1 nyumbani mbele ya CS Sfaxien na Simba ikapata ushindi wa bao 1-0 ziliporudiana huko Tunisia na baada ya hapo ni sare ya leo.

Kwa kupata bao leo, Simba inakuwa imefunga bao katika mechi zote tano za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisjo msimu huu.