Simba yaanza na wageni sita, Yanga watatu

Muktasari:
- Hilo ni pambano ni la 10 kwa timu hizo katika Ngao ya Jamii, huku katika mechi tisa za awali Simba ikiwa na rekodi ya kushinda tano ikiwamo ya msimu uliopita na Yanga kushinda nne.
Kocha Miguel Gamondi wa Yanga ameanza na kikosi chenye sura tatu mpya tofauti, huku kocha wa Simba Fadlu Davids akiwa na nyota sita kati ya 13 waliosajiliwa hivi karibuni, lakini sapraizi ni kipa Moussa Camara akikadhibiwa jezi namba 28 iliyokuwa ikitumiwa na kipa namba moja wa timu hiyo Aishi Manula.
Manula aliyesahaulika katika utambulisho wa kikosi hicho cha Msimbazi katika Tamasha la Simba Day, katika maisha yake ya soka tangu akiwa Azam hadi aliposajiliwa Simba mwaka 2017 alikuwa akiitumia namba hiyo 28 ambayo katika utambulisho wa kikosi kinachoanza jioni hii amevishwa Camara aliyetua wiki hii.
Kipa huyo kutoka Guinea ndiye aliyeanzishwa langoni akiwa mmoja ya nyota wapya sita waliosajiliwa na timu hiyo, wengine wakianzishwa katika pambano hilo ni beki Chamou Karabou na eneo la mbele likiwa na Debora Mavambo, Joshua Mutale, Charles Ahoua na Steven Mukwala likiwa ni eneo ambalo Simba imefanya mabadiliko makubwa.
Kwa upande was Yanga kocha Gamondi ameanza na Chadrack Boka katika nafasi ya Nickson Kibabage, huku Duke Abuya akicheza sehemu na Mudathir Yahya, huku Prince Dube akianzia sehemu ya Clement Mzize.
Hilo ni pambano ni la 10 kwa timu hizo katika Ngao ya Jamii, huku katika mechi tisa za awali Simba ikiwa na rekodi ya kushinda tano ikiwamo ya msimu uliopita na Yanga kushinda nne.
Vikosi vilivyo
YANGA: Diarra, Yao, Boka, Bacca, Job, Aucho, Maxi, Abuya, Dube, Aziz KI na Pacome
SIMBA: Camara, Kapombe, Tshabalala,Che Malone, Chamou, Mzamiru, Balua, Debora, Mukwala, Ahoua na Mutale