Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Queens kwenda fainali

Muktasari:

  • Kinara wa Kundi A, CBE ya Ethiopia ambao ndio wenyeji wenyewe watacheza mechi nyingine ya nusu fainali dhidi ya Kawembe Muslim ya Uganda iliyokuwa ya pili katika Kundi B nyuma ya Simba.


Dar es Salaam. Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Simba Queens inashuka tena uwanjani leo kuvaana na Kenya Police Bullets katika mechi ya nusu fainali ikiwa vita ya kusaka tiketi ya kucheza Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya pili.

Pambano hilo litapigwa kwenye Uwanja wa Abebe Bikila baada ya Simba kuongoza msimamo wa Kundi B ikivuna jumla ya pointi saba katika mechi tatu za kundi hilo, ikifunga mabao 10 na kufungwa mawili tu, huku wapinzani wao wakimaliza nafasi ya pili katika Kundi A ikiwa na pointi tisa.

Kinara wa Kundi A, CBE ya Ethiopia ambao ndio wenyeji wenyewe watacheza mechi nyingine ya nusu fainali dhidi ya Kawembe Muslim ya Uganda iliyokuwa ya pili katika Kundi B nyuma ya Simba.

Kwenye kundi hilo Kawempe Muslim ya Uganda ilimaliza nafasi ya pili na pointi sita huku PVP Buyenzi ya Burundi nafasi ya tatu na pointi mbili na FAD Djibouti ikimaliza mkiani.

Washindi wa mechi hizo watavaana katika mchezo wa fainali kusaka bingwa na mwakilishi wa ukanda huo katika fainali za CAF ambazo Simba ilishiriki mwaka 2022 na kumaliza ya nne kwa kufika nusu fainali, huku mwaka jana JKT Queens ilishiriki baada ya kutwaa ubingwa wa Cecafa, lakini ikaishia makundi.

Kocha wa Simba Queens, Juma Mgunda alisema mchezo wa leo sio rahisi kwa upande wao kama watu wanavyofikiria kwa sababu timu zote zimejiandaa.

"Tumecheza mechi tatu za makundi tumefunga mabao 10 zote hazikuwa rahisi tumesahau yaliyopita na sasa tunaingia kwenye mechi ya nusu fainali ambayo ukifanya makosa tu unatolewa hivyo tumejiandaa na tupo tayari kwa mchezo," alisema Mgunda.

Katika mechi hiyo Simba itaendelea kutegemea huduma za Asha Rashid 'Mwalala' na Mkenya Jentrix Shikangwa wenye mabao matatu kila moja sambamba na Viviasn Corazone katika kampeni ya kulibeba kwa mara ya pili ubingwa wa michuano hiyo ya Cecafa.