Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saliba afichua siri ya kuikataa Real Madrid na kubaki Arsenal

Muktasari:

  • Saliba alijiunga na Arsenal mwaka 2019 akitokea Saint Etienne ya Ufaransa.

Beki wa Arsenal, William Saliba ametaja sababu ambayo imefanya apige chini ofa ya kujiunga na Real Madrid ya Hispania na kubaki Arsenal hadi 2032.

Saliba amesema kuwa ameamua kusalia katika klabu ya Arsenal kwa vile anataka kushinda mataji akiwa anaitumikia jezi yake na sio kwenda kuyatafuta kwingine.

Beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24, leo Jumanne, Septemba 30 amesaini mkataba wa miaka mitano.

Kuongeza mkataba kwa Saliba ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa unafikia tamati 2027, kunaonekana kuikata maini Real Madrid ambayo imekuwa ikimuwania beki huyo kwa muda mrefu.

Saliba amesema kuwa asingeweza kujiunga na Real Madrid kama alivyofanya beki wa Liverpool, Trent Alexander-Arnord kwa vile bado hajashinda mataji na Arsenal.

“Me sijashinda mataji hapa. Nimeshinda Ngao ya Jamii pekee. Sijafanya chochote kwa klabu hii (Arsenal) hivyo sifikirii kuondoka. Nataka kuwepo hapa na kushinda mataji mengi.

“Naipenda klabu hii. Siwezi kuondoka pasipo kuipatia kitu chochote. Sijashinda chochote. Chaguo langu la kwanza lilikuwa ni kubaki hapa na kushinda kila kitu kwanza,” amesema Saliba.

Saliba alijiunga na Arsenal, Julai 2019 lakini baada ya meneja Mikel Arteta kuanza kuinoa timu hiyo, kuanzia Desemba 2019 alitolewa kwa mkopo mara tatu tofauti hadi 2022 aliporudishwa rasmi na kujihakikishia nafasi kikosi cha kwanza hadi sasa.

Saliba anafichua kwamba Arteta alimuweka wazi kuwa uamuzi huo ulilenga kumsaidia yeye mwenyewe na umechangia kwa kiasi kikubwa awe bora.

“Alikuwa wazi kwangu. Wiki ya kwanza aliniambia kuwa sipo tayari kucheza. Nilikuwa nafanya mazoezi na kucheza na kikosi cha umri chini ya miaka 21.

“Mwishoni mwa Desemba aliniambia ni bora kwangu niende kwa mkopo kuliko kukaa bila kucheza. Nilikuwa na hasira kwa sababu nilihitaji kucheza.

“Baada ya mkopo wa kwanza aliniambia nahitajika kwenda mkopo wa pili. Sikukata tamaa na leo hii nipo hapa mbele yako naichezea Arsenal,” amesema Saliba.