Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la Yanga kutumia nyumba Isamuhyo yatozwa mamilioni


Muktasari:

  • klabu hiyo imepigwa faini ya Sh30 milioni kwa kosa la wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia na badala yake kutumia nyumba iliyokuwa nje ya eneo la uwanja.

Dar es Salaam. Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh30 milioni na kupewa onyo kali na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kufuatia makosa mbalimbali yaliyotokea katika mchezo dhidi ya Simba SC uliochezwa Mei 3, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Mei 11, 2026 na TPLB, Yanga imepewa onyo kali kwa kuchelewa kuwasili uwanjani kwa dakika tano, baada ya kufika saa 10:35 alasiri badala ya saa 10:30.

Mbali na onyo hilo, klabu hiyo imepigwa faini ya Sh30 milioni kwa kosa la wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia na badala yake kutumia nyumba iliyokuwa nje ya eneo la uwanja.

Katika mchezo huo Yanga iliilazimisha Simba sare ya mabao 2-2 na kuendelea kuweka hai matumaini yake ya kutetea ubingwa wa ligi.

Kamati hiyo pia imemfungia idadi ya mechi tatu, Meneja wa Yanga, Walter Harrison na kumtoza faini ya Sh1 milioni kwa kosa la kumsukuma mchezaji wa Simba, Clatous Chama.

Pia shabiki wa Yanga, aliyetambulika kwa jina la Mohamed Ally Mposo amefungiwa kuingia uwanjani kwa miezi 12 kwa kosa la kuingia katika eneo la kuchezea na kumwaga vimiminika, kitendo kilichotafsiriwa kama imani za kishirikina.

Ukiondoa adhabu hizo zilizoihusu Yanga, Dodoma Jiji imetozwa faini ya Sh5 milioni kwa kosa la kuchelewa kufika katika kikao cha maandalizi ya mchezo huku wakiwa pungufu bila vifaa vyote vinavyohitajika.

Kosa hilo limefanywa katika mchezo namba 154 dhidi ya Mtibwa Sugar.