Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo JR kucheza na baba yake

Mshambuliaji wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo akiwa na mwanaye Cristiano Ronaldo Jr. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Orodha hiyo inawajumuisha Rivaldo na mwanaye Rivaldinho, Henrik Larsson na mwanaye Jordan Larsson, pamoja na George Eastham Sr na George Eastham Jr wa miaka ya 1950.

Riyadh. Mtoto wa Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 16, anaripotiwa kuandaliwa kuingizwa haraka katika kikosi cha kwanza cha klabu ya Al-Nassr.

Cristiano Ronaldo Jr anaweza kujikuta akicheza uwanjani pamoja na baba yake siku za karibuni, huku klabu ya Al-Nassr ikifikiria kumpandisha haraka katika mazoezi ya kikosi cha kwanza msimu ujao.

Ronaldo, ambaye sasa ana miaka 41, kwa muda mrefu ameonyesha hamu yake ya siku moja kucheza soka la kulipwa pamoja na mwanaye mkubwa, ambaye anaendelea kukua kisoka baada ya kuiwakilisha Manchester United na na timu ya Taifa ya Ureno katika ngazi za vijana.

Kijana huyo alimfuata baba yake kwenda Saudi Arabia mwaka 2023 na kwa sasa anacheza katika akademi ya Al-Nassr, lakini ripoti kutoka Saudi Arabia zinaeleza kuwa viongozi wa klabu hiyo wanatafakari kumpandisha mshambuliaji huyo kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza kwa msimu wa 2026/27.

Mapema mwaka huu, Ronaldo aliyewahi kuichezea Real Madrid na Manchester United, alisema muda unaendelea kuyoyoma katika kutimiza ndoto yake ya kuwa miongoni mwa kundi maalum la baba waliowahi kucheza soka la kulipwa pamoja na watoto wao.

Orodha hiyo inawajumuisha Rivaldo na mwanaye Rivaldinho, Henrik Larsson na mwanaye Jordan Larsson, pamoja na George Eastham Sr na George Eastham Jr wa miaka ya 1950.

Alisema: “Ningependa hilo litokee, ningependa. Sio jambo linaloninyima usingizi, lakini ningependa. Tutaona. Ni zaidi mikononi mwake kuliko yangu. Miaka inaendelea kusonga na bila shaka siku moja nitalazimika kuacha soka kwa sababu muda ninaouongeza utafika wakati ambapo haitawezekana tena.

Picha na Mtandao.

“Sio tu kimwili bali pia kisaikolojia. Lakini pia sioni kama ni jambo la lazima. Atafuata njia yake, mkondo wake. Nitakuwa baba mwenye fahari kwa chochote atakachochagua kufanya. Akicheza, sawa kabisa. Asipoicheza, tulijaribu. Angalau baba yake alijitahidi sana. Lakini haitakuwa tatizo pia, kwa maoni yangu.”

Ronaldo Jr ni mshambuliaji kama baba yake na anaweza kucheza pembeni au katikati ya safu ya ushambuliaji.''

Mapema mwaka huu pia iliripotiwa kuwa kijana huyo mwenye miaka 16 aliwahi kufanya mazoezi na akademi ya Real Madrid, akitazamiwa uwezekano wa kuhamia Hispania siku zijazo.

Ingawa alizaliwa nchini Marekani, Ronaldo Jr amechagua kuiwakilisha Ureno, na alipata mwaliko wake wa kwanza kwenye kikosi cha vijana Mei mwaka jana.

Alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Japani katika mashindano ya Vlatko Markovic International Tournament na tangu hapo ameendelea kuiwakilisha nchi yake katika kiwango cha chini ya miaka 17.