Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo apewa mkataba wa kufuru Al-Nassr

Riyadh, Saudi Arabia. Nyota wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, ameandika historia mpya katika mchezo huo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia wenye thamani ya Pauni Milioni 492 (Sh1.6 trilioni), huku ukitajwa kuwa mkataba wa gharama kubwa zaidi katika historia ya michezo duniani.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, nyongeza hiyo ya mkataba inampa mshahara wa hadi Pauni 488,000 kwa siku (Sh1.6 bilioni), na pia kumfanya kuwa balozi rasmi wa ndoto za maendeleo ya taifa hilo la Ghuba, hatua ambayo inaweza kupandisha jumla ya mapato yake hadi zaidi ya Pauni Milioni 500 ndani ya miaka miwili.

Mkataba huo, unaomfikisha hadi baada ya kutimiza miaka 42, pia unampa Ronaldo bonasi ya usajili ya Pauni Milioni 24.5 (Sh80 bilioni) ambayo inaweza kufikia Pauni Milioni 38 endapo atakamilisha mwaka wa pili wa mkataba huo.

Ripoti hiyo pia inasema Ronaldo amepewa umiliki wa asilimia 15 wa Al-Nassr sawa na thamani ya Pauni Milioni 33 ikiwa ni mara ya kwanza kwa mchezaji kupata nafasi ya kuwa sehemu ya wamiliki wa klabu hiyo. Aidha, Ronaldo ataongeza kipato chake zaidi iwapo atatwaa tuzo ya mfungaji bora au kusaidia Al-Nassr kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Taarifa rasmi za kusaini mkataba huo mpya zilitolewa Alhamisi, zikifuatia miezi ya uvumi uliokuwa ukieleza kuwa anaweza kuondoka klabuni hapo kufuatia msimu mwingine wa kukosa taji. Mwezi uliopita, Ronaldo aliibua sintofahamu kwa kuchapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii uliosomeka “sura hii imefungwa,” ukitafsiriwa kama ishara ya kuaga Al-Nassr.

Hata hivyo, baada ya kuiongoza Ureno kutwaa ushindi kwenye UEFA Nations League, Ronaldo (40) alithibitisha kuwa atarejea kuichezea Al-Nassr msimu ujao, akichapisha kwenye akaunti yake ya X (zamani Twitter): “Sura mpya inaanza. Shauku ileile, ndoto ileile. Hebu tuandike historia pamoja.”

Katika msimu uliopita, Ronaldo alifunga mabao 35 katika mechi 41 kwenye mashindano yote, na kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia kwa msimu wa pili mfululizo. Tangu ajiunge na klabu hiyo Desemba 2022 akitokea Manchester United, amefunga jumla ya mabao 99 katika mechi 111, na sasa yupo hatua chache kufikia lengo lake la mabao 1,000 katika soka la ushindani akiwa tayari na mabao 938.

Mbali na fedha, maisha ya Ronaldo nchini Saudi Arabia yamewekewa mazingira bora zaidi. Klabu hiyo itagharamia huduma ya watumishi 16 wa kudumu kwa familia yake, wakiwemo madereva watatu, wapishi wawili, walinzi wanne, wasaidizi wa nyumbani wanne na wapishi wawili wote watalipwa Pauni Milioni 1.4 (Sh4.7 bilioni).

Aidha, Ronaldo amewekewa matumizi ya ndege binafsi yenye thamani ya Pauni Milioni 4 (Sh13 bilioni), pamoja na fursa ya mikataba ya udhamini na makampuni ya Kisaudi ambayo inaweza kufikia hadi Pauni Milioni 60.

Chanzo kutoka ndani ya klabu hiyo kimeeleza kuwa kulikuwa na hofu kubwa kuwa mchezaji huyo aliyeshinda Ballon d’Or mara tano na ambaye anachukuliwa kuwa uso wa ligi hiyo, angeondoka. Hata hivyo, hatua ya kusaini mkataba mpya imeondoa hofu hiyo.

Habari za mkataba huu zimekuja siku moja tu baada ya kuthibitishwa kuwa kocha mkuu Stefano Pioli ataondoka klabuni hapo. Pioli anakuwa kocha wa nne kuondoka Al-Nassr tangu Ronaldo ajiunge nayo Januari 2023, akifuata nyayo za Rudi Garcia, Dinko Jelicic na Luís Castro.

Akituma salamu za kuagana na kocha huyo kupitia X, Ronaldo aliandika kwa Kitaliano: “Grazie per tutto,” akimaanisha “Asante kwa yote.”