Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford ashinda taji la kwanza Barcelona

Muktasari:

  • Barcelona imeanza mchakato wa kumchukua Rashford moja kwa moja.

Marcus Rashford ameonja ladha ya mafanikio kwa mara ya kwanza akiwa na jezi ya Barcelona baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wapinzani wao Real Madrid katika fainali ya Kombe la Super la Hispania.

Mshambuliaji huyo raia wa England aliingia uwanjani dakika ya 83 akichukua nafasi ya Raphinha aliyefunga mabao mawili.

Katika mchezo huo wa mkali uliofanyika huko mjini Jeddah, Saudi Arabia. Rashford alikaribia kufunga bao la nne dakika za mwisho za mchezo, lakini shuti lake lilipaa nje kidogo.

Ushindi huo umekuja wakati klabu yake ya zamani Manchester United ikiondolewa kwenye Kombe la FA, hali iliyozidi kuumiza mashabiki wa timu hiyo baada ya kutolewa mapema kwenye mashindano yote ya ndani kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1981/82.

Rashford, 28, alijiunga na Barcelona kwa mkopo kutoka Manchester United kufuatia mvutano na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Ruben Amorim. Tangu awasili Hispania, amefunga mabao saba katika michezo 27 aliyocheza, akianza benchi katika michezo 10.

Katika fainali hiyo, Raphinha alifunga mabao mawili huku Robert Lewandowski naye akiandika jina lake kwenye orodha ya wafungaji. Kwa upande wa Real Madrid, Gonzalo Garcia na Vinicius Jr walifunga mabao yao, lakini haikutosha kuizuia Barcelona kutwaa taji hilo, licha ya Frenkie de Jong kuonyeshwa kadi nyekundu dakika za mwisho.

Taarifa zinaeleza kuwa, licha ya kuondoka kwa Amorim Manchester United, bado hakuna dalili za Rashford kurejea Old Trafford. Badala yake, Barcelona inaelezwa kuwa tayari kuanzisha mchakato wa kumchukua moja kwa moja kwa ada ya pauni 26 milioni, ingawa huenda ikajaribu kujadiliana kupunguza kiasi hicho.

Endapo dili hilo litakamilika, litahitimisha safari ya miaka 21 ya Rashford ndani ya Manchester United, ambako alishinda Kombe la FA na Ligi ya Europa.

Akizungumza na chombo cha habari cha Hispania, Sport, Rashford amesema anatamani kuendelea na Barcelona na kushiriki katika mipango ya kushinda mataji zaidi.

“Barcelona ni klabu kubwa inayopenda ushindi. Hii ni aina ya presha ninayoitaka. Nimekuja hapa kusaidia timu kushinda mataji na nipo tayari kufanya kazi kwa bidii,” alisema Rashford.

Ushindi huo unaipa Barcelona matumaini ya kuanza msimu kwa mafanikio makubwa zaidi, huku Rashford akionekana kuanza ukurasa mpya wenye matumaini katika maisha yake ya soka.