Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG, Bayern zaacha rekodi usiku wa Ulaya

Muktasari:

  • Ushindi wa mabao 5-4 ilioupata PSG mbele ya Bayern hatua ya nusu fainali, umeweka rekodi ya kuwa mechi iliyozaa mabao mengi kila upande katika michuano hiyo kutokana na timu moja kufunga mabao matano, huku hiyohiyo pia ikiruhusu manne.

PSG na Bayern Munich zimeoneshana ubabe ndani ya dakika 90 zilizoacha rekodi kabambe katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

Ushindi wa mabao 5-4 ilioupata PSG mbele ya Bayern katika hatua ya nusu fainali, umeweka rekodi ya kuwa mechi iliyozaa mabao mengi kila upande katika michuano hiyo kutokana na timu moja kufunga mabao matano, huku hiyohiyo pia ikiruhusu manne.

Si hatua ya makundi wala mtoano, haikuwahi kutokea ndani ya dakika 90 hali ikawa hivyo, zaidi imeshuhudiwa vipigo vikubwa kama Liverpool 8-0 Beşiktaş, Real Madrid 8-0 Malmö na Bayern 9-2 GNK Dinamo.

Bayern Munich italazimika kupambana kurejea katika mchezo wa marudiano ikiwa inataka kufuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa mabao 5-4 na Paris Saint-Germain katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana Jumanne Aprili 28, 2026.

Harry Kane, Michael Olise, Dayot Upamecano na Luis Diaz waliifungia Bayern katika mchezo huo uliokuwa wa piga nikupige.

Bayern walianza mchezo kwa kasi na walipata bao la kuongoza baada ya Diaz kuangushwa ndani ya eneo la hatari na Willian Pacho, ambapo Kane hakukosea mkwaju wa penalti. Baadaye Olise alipata nafasi nzuri ya kuongeza bao la pili, lakini shuti lake dhaifu liliokolewa kwa juhudi za Matvey Safonov na Marquinhos.

Nyota wa PSG, Khvicha Kvaratskhelia wakati akishangilia moja ya bao katika ushindi wa 5-4 iliopata PSG dhidi ya Bayern katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Aprili 28,2026. Picha na Mtandao

PSG waliinuka na kuanza kucheza vizuri, na muda mfupi baada ya Ousmane Dembele kukosa nafasi ya wazi, Khvicha Kvaratskhelia alifanya juhudi nzuri kwa kukata ndani kutoka upande wa kushoto na kupiga shuti lililoingia kona ya chini ya goli.

Joao Neves aliipa PSG bao la pili kwa kichwa baada ya kona, muda mfupi tu baada ya yeye mwenyewe kupiga mpira uliogonga mwamba kufuatia krosi ya Olise.

Olise alipata bao lake kwa shuti kali kutoka katikati lililompita Safonov, lakini PSG walirejea tena kuongoza mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya Dembele kufunga penalti kufuatia Alphonso Davies kuonekana kushika mpira akiwa eneo la hatari.

PSG walionekana kuanza kutawala mchezo huo baada ya mapumziko, ambapo Kvaratskhelia na Dembele waliongeza mabao yao kwa haraka.

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Luis Diaz wakati akifunga moja ya bao katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyomalizika kwa PSG kushinda 5-4 Aprili 28, 2026. Picha na Mtandao

Hata hivyo, Bayern hawakukata tamaa, na Upamecano alipata mguso mdogo kwenye mpira wa adhabu uliopigwa na Joshua Kimmich na kufunga, kabla ya Diaz kutumia pasi ndefu ya Kane kufunga bao jingine.

Timu zote mbili zilipata nafasi za kuongeza mabao, huku Senny Mayulu akipiga mpira uliogonga mwamba na Kimmich pia akishuhudia kichwa chake kikitolewa kwenye mstari wa goli na Pacho katika dakika za mwisho.

Mwisho wa siku, kila kitu kipo wazi kuelekea mchezo wa marudiano utakaochezwa kwenye uwanja wa Allianz Arena huko Ujerumani Jumatano ijayo, ukiwa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.