Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atletico Madrid, PSG zatinga nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya

Muktasari:

  • Hii ni mara ya kwanza kwa Atletico Madrid kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu ilipofanya hivyo msimu wa 2016/2017.

Atletico Madrid na PSG zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu baada ya kupata matokeo zilizokuwa zinayahitaji katika mechi zilizochezwa jana Jumanne, Aprili 14, 2026.

Jijini Madrid, wenyeji Atletico Madrid licha ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Barcelona, wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 wakibebwa na ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mechi ya kwanza ugenini.

Mabao ya Lamine Yamal na Ferran Torres yalionekana kama yangeweza kuibeba Barcelona lakini Ademola Lookman alipachika bao moja ambalo limeihakikishia Atletico kusonga mbele na sasa inaisubiria timu itakayosonga mbele baina ya Arsenal na Sporting Lisbon.

Katika mchezo huo, Eric Garcia ameonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 79 kwa kosa la kumfanyia faulo, Alexander Sorloth aliyekuwa anaelekea kufunga.

Hii ni mara ya kwanza kwa Atletico Madrid kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu ilipofanya hivyo msimu wa 2016/2017.

Jijini Liverpool, wenyeji Liverpool wametoka kichwa chini baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa PSG.

Mabao mawili ya Ousmane Dembele katika Uwanja wa Anfield yamemaanisha kuwa Liverpool imega mashindano hayo kwa kichapo cha jumla cha mabao 4-0 kwani katika mechi ya kwanza ilifungwa mabao 2-0 ugenini.

PSG sasa inamngojea mshindi wa jumla kati ya Bayern Munich au Real Madrid ili ikutane naye katika hatua ya nusu fainali.

Baadaye leo Jumatano, kutakuwa na michezo miwili ambayo ni Bayern dhidi ya Real Madrid na Arsenal dhidi ya Sporting Lisbon.

Katika mechi ya kwanza, Real Madrid ilifungwa mabao 2-1 na Sporting Lisbon yenyewe ilichapwa bao 1-0.