Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Stars waahidi ushindi kwa DR Congo

Muktasari:

  • Ili Taifa Stars iingie hatua ya 16 bora, inahitajika kupata ushindi katika mchezo wa kesho Januari 24, 2024 na kisha kuombea Zambia ipoteze au itoke sare na Morocco katika mechi ya mwisho ili yenyewe itinge 16 bora.

Wakati wachezaji na benchi la ufundi la Taifa Stars wakiipigia hesabu kali mechi ya mwisho ya kundi F la Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 dhidi ya DR Congo kesho katika Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly, kocha mzoefu ameishauri cha kufanya ili ipate ushindi katika mechi hiyo.

Sare ya bao 1-1 ambayo ilipata dhidi ya Zambia juzi Jumapili, imeifanya Taifa Stars kuwa mkiani mwa msimamo wa kundi F ikiwa na pointi moja nyuma ya kinara Morocco yenye pointi nne na ikifuatiwa na DR Congo na Zambia ambazo kila moja ina pointi mbili.

Ili Taifa Stars iingie hatua ya 16 bora, inahitajika kupata ushindi katika mchezo wa kesho Januari 24, 2024 na kisha kuombea Zambia ipoteze au itoke sare na Morocco katika mechi ya mwisho ili yenyewe itinge 16 bora.

Lakini hilo likishindikana, Taifa Stars inaweza kupenya kupitia tiketi ya timu nne shindwa (best losers), lakini bado hata hivyo itapaswa kuibuka na ushindi dhidi ya DR Congo.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema watahakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya DR Congo, kwani mechi hiyo imeshikilia hatima yao kwenye fainali hizo.

"Bado tuna mchezo mmoja ambao inabidi tupambane ili tupate ushindi ili kuangalia kama tunaweza kusonga mbele," amesema Samatta.

Mshambuliaji Saimon Msuva amesema,"Tuna nafasi katika mchezo unaofuata. Hautokuwa mwepesi kwetu, lakini naamini tutafanya vizuri. Sisi hatutachoka na tunaendelea kuhimizana," amesema Msuva.

Kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars, Hemed Morocco ambaye ana uzoefu na michuano hiyo amesema wanajipanga kuhakikisha DR Congo hatoki salama katika mechi hiyo.

"Siku hizi mpira umebadilika na hakuna mdogo tena, hivyo sisi tunajipanga vizuri huku tukiamini tunaweza kupata matokeo mazuri kwenye mechi hii."

Kocha wa Tabora United, Goran Kuponovic amesema Stars inaangushwa na kukosa kundi kubwa la wachezaji wa daraja la juu, hivyo Tanzania inapaswa kupambana kuhakikisha inapeleka wanasoka wengi kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

"Kwenye haya mashindano Stars inaponzwa kwa kuwa wachezaji wake wengi wanazichezea timu za kawaida tofauti na wapinzani wao Morocco, Zambia na hata Congo. Naona Mbwana Samatta ndiye anacheza klabu kubwa Ulaya, hivyo ni vyema sasa ukawekwa mkakati wa kuzalisha vijana wapya."