Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni Nigeria, DR Congo Fainali Mchujo Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Mabao sita yamefungwa katika mechi mbili za hatua ya nusu fainali ya mchujo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia kupitia Kanda ya Afrika.

Nigeria na DR Congo zitakutana katika mechi ya Fainali ya hatua ya kwanza ya mchujo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia baada ya jana kupata ushindi katika mechi za nusu fainali zilizochezwa usiku, Rabat, Morocco.

Mshindi wa mechi hiyo ya Fainali atapata tiketi ya kuiwakilisha Afrika katika hatua ya mwisho ya mchujo itakayokutanisha timu sita kutoka mabara matano tofauti duniani ambazo zitawania tiketi mbili za kucheza Kombe la Dunia 2026 huko Canada, Mexico na Marekani.

Nigeria imepata tiketi ya Fainali ya Mchujo kwa upande wa bara la Afrika baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Gabon katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye Uwanja wa Prince Mourlay, Rabat.

Iliwalazimu Nigeria kusubiri hadi katika dakika 30 za nyongeza kupata ushindi huo baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika kwa sare ya bao 1–1.

Akor Adams alianza kuifungia bao Nigeria katika dakika ya 78 lakini dakika ya 89, Gabon walisawazisha kupitia kwa Mario Lemina.

Gabon walikiona cha moto katika dakika 30 za nyongeza ambazo Nigeria walizitumia vyema kupata mabao matatu kupitia kwa Victor Osimhen aliyepachika mabao mawili na lingine moja likifungwa na Chidera Ojuke.

Kwenye nusu fainali nyingine iliyofanyika katika Uwanja wa Al Barid, DR Congo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cameroon, yenyewe ikimaliza mechi katika dakika 90.

Bao la ushindi la DR Congo katika mchezo huo limefungwa katika dakika za majeruhi na Chancel Mbemba aliyeunganisha kwa shuti la mguu wa kulia mpira wa kona wa Brian Cipenga.

Mchezo wa Fainali baina ya Nigeria na DR Congo utachezwa keshokutwa Jumapili katika Uwanja wa Prince Mourlay Hassan, Rabat.