Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nado, Kagoma watemwa Taifa Stars, Azam wakitawala kikosi

Muktasari:

  • Taifa Stars itacheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Uganda na Rwanda zitakazochezwa Juni mwaka huu huko Morocco.

Wachezaji Iddi Selemani ‘Nado’ na Yusuph Kagoma wamewekwa kando katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitakachocheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki mwezi ujao dhidi ya Uganda na Rwanda huko Morocco.

Wawili hao walikuwepo katika kikosi cha Taifa Stars kilichoshika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya FIFA Series, Machi mwaka huu.

Ukiondoa hao, wengine ambao walikuwepo kwenye FIFA Series na hawajaitwa kikosini safari hii ni Kelvin Nashoni wa Pamba Jiji, Kelvin John (Aalborg) na Paul Peter (JKT Tanzania).

Azam FC ndio timu iliyotawala kikosi hicho cha sasa cha Taifa Stars, ikitoa wachezaji watano.

Kwa mara nyingine tena, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi hajamjumuisha nyota wa Le Havre ya Ufaransa na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.

Kiwango bora cha nyota wa Coastal Union, Bakari Msimu kimemfanya aendelee kuaminiwa na Kocha Gamondi.

Kuna urejeo wa nyota wa kimataifa wa Tanzania anayecheza Eastbourne ya England, Mohammed Sagaf ambaye hajaitwa katika kikosi cha Taifa Stars kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Wachezaji wanaounda kikosi cha Taifa Stars kilichotangazwa leo, Jumapili, Mei 24, 2026 ni Aishi Manula, Zuber Foba, Pascal Msindo, Elias Lawi na Feisal Salum (Azam), Ibrahim Hamad, Bakari Mwamnyeto na Mudathir Yahya (Yanga) na Nickson Kibabage, Vedastus Masinde na Selemani Mwalimu (Simba).

Pia wapo Yona Amos (Pamba Jiji), Mohamed Mussa (Mashujaa), Abdulkarim Kiswanya (Namungo), Bakari Msimu (Coastal Union) na Haji Mnoga (Salford City).

Wengine ni Mohammed Sagaf (Eastbourne), Charles M’Mombwa (Floriana), Alphonce Mabula (Shamakh), Novatus Dismas (Goztepe), Tarryn Allarakhia (Rochdale), Saimon Msuva (Al Talaba), Cyprian Kachwele (HFX Wanderers) na Said Khamis (Immigration).