Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzize achaguliwa mchezaji bora CAF

Muktasari:

  • Kiwango cha mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize alichoonyesha katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya TP Mazembe kimempaisha na kuchaguliwa mchezaji bora wa wiki.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize (20) amechaguliwa na shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kuwa mchezaji bora wa wiki baada kuisaidia Yanga kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo huo, ilishuhudiwa Yanga ikitoka nyuma na kupata ushindi ambapo Mzize alipachika mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa huku akionyesha kiwango bora. CAF imemtangaza Mzize baada ya kuwashinda nyota wengine waliokuwa wakichuana kwenye orodha ya wachezaji waliofanya vizuri wiki hii.

Mabao mawili alioyafunga dhidi ya Mazembe yanamfanya kufikisha jumla ya mabao matatu kwenye mshindano haya msimu huu baada ya kucheza mechi tatu.

Mzize ambaye ameonyesha kiwango bora kwenye mchezo uliopita anaendelea kuvivutia Vilabu vikubwa hapa Afrika ambavyo vimekuwa vikiitaji huduma yake.

Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye kundi A ikiwa na pointi nne, nyuma ya  MC Alger iliyo nafasi yapili kwa  pointi tano na vinara Al Hilal wenye pointi 10, timu inayoburuza mkia ikiwa ni  TP Mazembe ambayo ina pointi mbili.

Mchezo unaofuata Yanga itasafiri kwenda Maurtania kuwakabili Al Hilal ya kocha, Florent Ibenge katika  mchezo utakaopigwa Januari 12, 2025.

Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na kisasi cha kulipa baada ya kupoteza mechi ya nyumbani iliyopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo ilichapika mabai  2-0.

Iwapo Yanga itapata ushindi dhidi ya Al Hilal itajiweka pazuri kufuzu hatua ya robo fainali kwani itahitaji kushinda mechi yao ya mwisho ya nyumbani  dhidi ya MC Alger Januari 18, 2025