Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu aiokoa Taifa Stars ugenini Congo

Muktasari:

  • Taifa Stars inashika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi E ikiwa na pointi 10.

Dar es Salaam. Bao la dakika ya 84 la Selemani Mwalimu limeiwezesha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kupata pointi moja muhimu katika mchezo wa ugenini dhidi ya Congo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026.

Mwalimu aliyeingia kutoka benchi kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya, alifunga bao hilo kwa shuti la wastani la mguu wa kulia akimalizia pasi ya Clement Mzize.

Ni mchezo ambao ulionekana kama Stars itaangusha pointi tatu baada ya Congo kutangulia kupata bao katika dakika ya 68 kupitia kwa Dejan Moussavou lakini mwalimu alibadili ubao wa matokeo, dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho.

Matokeo hayo ya leo yameifanya Taifa Stars kubakia katika nafasi ya pili ya kundi E ikifikisha pointi 10 huku Congo ikiendelea kushika mkia na pointi yake moja.

Taifa Stars sasa inahitajika kupata ushindi katika mechi mbili ilizobakiza dhidi ya Niger na Zambia ili kujaribu kusaka nafasi ya kufuzu kupitia mechi za mchujo.

Ikumbukwe katika kundi hilo, timu ambayo imeshafuzu ni Morocco ambayo inaongoza msimamo ikiwa na pointi 15.

Katika mchezo wa leo, kikosi kilichoanza cha Taifa Stars kiliundwa na Yakoub Suleiman, Shomari Kapombe, Paschal Msindo, Ibrahim Hamad, Dickson Job, Novatus Miroshi, Saimon Msuva, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta, Feisal Salum.

Baadaye waliingia Mwalimu, Iddi Seleman, Mohamed Hussein na Lusajo Mwaikenda.

Taifa Stars itaingia tena uwanjani, Jumanne Septemba 9, 2025 kukabiliana na Niger katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.