Mtanzania anayekipiga Ureno akinukisha

Muktasari:
Mechi hiyo ililenga kutambulisha jezi mpya watakazotumia katika ligi na mashindano ya Kombe la FA 'Taca da Liga' bingwa wa kombe hilo ataiwakilisha Ureno katika mashindano ya Europa Ligi.
Dar es Salaam. Mtanzania Orgenes Mollel (19) ameiongoza timu yake ya Famalicao inayoshiriki Ligi daraja la pili ‘LigaPro’, Ureno kupata suluhu na Braga B katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi hiyo.
Mechi hiyo ililenga kutambulisha jezi mpya watakazotumia katika ligi na mashindano ya Kombe la FA 'Taca da Liga' bingwa wa kombe hilo ataiwakilisha Ureno katika mashindano ya Europa Ligi.
“Ukiachilia mbali kuzindua jezi tutazozitumia msimu huu, pia mchezo maalumu kwa kujiandaa mechi ya Kombe la FA Jumapili.
“Kocha alitoa nafasi ya kucheza dakika 45 kwa kila mchezaji, nilicheza dakika 45 za kipindi cha kwanza na baada ya hapo nafasi yangu ilichukuliwa na mchezaji mwingine, lakini mchezo ulimalizika bila kufungana,” alisema Mollel.
Famalicao itaanzia nyumbani kwenye Uwanja wa Municipal 22 de Junho kucheza dhidi ya Santa Clara katika hatua ya mzunguko wa kwanza.