Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msuva aipa Iran bao lake

Mshambuliaji wa Al Talaba, Simon Msuva wakati akifunga moja ya bao katika Ligi Kuu nchini Iraq. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Bao hilo linakuwa la tatu kwa Msuva msimu huu ishara kuwa winga huyo ambaye alikuwa na Taifa Stars kwenye michuano ya AFCON 2025 bado anaendelea kuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho

Winga wa Tanzania, Simon Msuva anayekipiga Al Talaba ameendelea kuonyesha kiwango bora katika Ligi Kuu ya Iraq baada ya kufunga bao muhimu na kisha kulitoa zawadi kwa taifa la Iran huku akiomba hali ya amani irejee katika eneo hilo.

Msuva alifunga bao hilo katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Al Qassim kwenye mechi ya ligi iliyopigwa katika mazingira yaliyoelezwa kuwa na presha kutokana na hali ya usalama inayoendelea kuripotiwa kwenye ukanda huo kutokana na kuzuka vita kati ya Iran, Israel na Marekani baada ya mvutano wa muda mrefu ambapo mpaka sasa watu kadhaa wameripotiwa kufariki na baadhi ya miji kuharibiwa vibaya.

Bao hilo liliwashangaza mabeki wa Al Qassim kutokana na alivyopiga mpira wa kichwa uliotokana na krosi na kumshinda kipa aliyebaki akiutazama ukijaa nyavuni.

Akizungumza na Mwananchi, Msuva amesema ameamua kulitoa bao hilo kwa wananchi wa Iran huku akiomba hali itulie haraka kwa sababu ikiendelea hivyo inaweza kuathiri hata mwenendo wa ligi.

“Nimelitoa goli hili kwa Iran, tunaomba mambo yawe sawa haraka kwa sababu hali ikiendelea hivi inaweza kuleta changamoto kubwa hata kwa ligi kuendelea.”

Ameongeza katika kipindi hiki cha machafuko amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka kujua hali yake ya usalama, akisisitiza kwa sasa yuko salama na anaendelea na majukumu yake ya soka.

“Watu wengi wamekuwa wakinipigia simu kuniuliza hali yangu ya usalama, lakini namshukuru Mungu niko vizuri na naendelea na kazi yangu,” alisema Msuva.

Ushindi huo umeifanya Talaba isogee hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 40 katika mechi 21 ilizocheza.

Bao hilo linakuwa la tatu kwa Msuva msimu huu ishara kuwa winga huyo ambaye alikuwa na Taifa Stars kwenye michuano ya AFCON 2025 bado anaendelea kuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho licha ya ushindani mkubwa uliopo katika ligi hiyo.