Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappé kuvuliwa jezi namba tisa Madrid

Muktasari:

  • Kinda wa timu hiyo kutokea Brazil, Endrick ndiye anatajwa kuvaa jezi hiyo msimu ujao.

Madrid, Hispania. Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappé ataachana na jezi namba tisa mgongoni ambayo amekuwa akiitumia katika msimu wake wa kwanza wa 2024-2025.

Madrid imepanga kumpa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ikitumiwa na Luca Modric ambaye amethibitisha kuondoka klabuni hapo msimu huu.

Licha ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kuonyesha kiwango kizuri msimu huu akiwa na jezi namba tisa mgongoni, Real Madrid inaamini jezi namba 10 itakuwa bora zaidi kwa nyota huyo hususani katika kufanya biashara ya uuzaji wa jezi ambapo jezi namba 10 imekuwa nembo muhimu kwa mastaa wa soka duniani.

Hata hivyo, katika mkataba wake na Madrid alitakiwa apewa jezi hiyo mwanzoni mwa msimu huu lakini kwa kumheshimu Luca Modric hakuweza kumvua jezi mkongwe huyo ambapo amesubiri mpaka kuondoka kwake.

Taarifa kutoka Madrid zinaeleza kwamba baada ya Mbappe kuachia jezi namba tisa msimu ujao, kinda wa timu hiyo kutokea Brazil, Endrick ndiye anatajwa kuvaa jezi hiyo.

Mbappe amefunga jumla ya mabao 42 katika msimu wake wa kwanza akiwa na wababe hao wa Ulaya ambapo ameibuka kuwa mfungaji bora wa La Liga pamoja na mfungaji bora mwenye mabao mengi zaidi Ulaya akiwaacha Mohamed Salah wa Liverpool na Victor Gyokeres wa Sporting CP waliokuwa wapinzani wake wa karibu.