Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabululu azua kihoja kwa Mkapa, walinzi wamuondoa

Mshambuliaji wa Al Ahly Tripoli,  Cristovao Paciencia Mabululu amezua kihoja kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa baada ya kuonekana akikagua nje kabisa ya eneo la kuchezea kwa kunyanyua nyavu na kuchomoa vibendera kuangalia kama kuna kitu kimewekwa.

Tukio hilo limetokea muda mchache kabla ya wachezaji kupasha misuli ikiwa ni utaratibu maalumu kwa wachezaji kutazama uwanja kabla ya kurejea kwenye vyumba vya kubadilisha nguo na kuwa tayari kwa maezoezi mepesi.

Hata hivyo, kitendo hicho ambacho ni kinyume na taratibu kiligundulika haraka na walinzi watatu wa uwanjani ambao walimkimbilia na kumuondoa.

Kitendo hicho, Mabululu aloneakana kukifanya upande ambao Simba iliutumia kupasha misuli na hata wakati akiondolewa alionekana mwenye kujiamini kabla ya ofisa wa timu yake kumkimbilia kwa ajili ya kumsapoti.

Wekundu wa Msimbazi, Simba wapo nyumbani kumalizana na Walibya hao kwenye Kombe la Shirikisho Afrika  baada ya mchezo wa kwanza kutoka suluhu wakiwa ugenini wikiendi iliyopita.