Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yapigwa, Southampton yashuka

Liverpool, England. Liverpool ikiwa ugenini imepoteza mchezo wa pili msimu huu baada ya kulala kwa mabao 3-2 dhidi ya Fulham.

Liverpool ilikuwa inapewa nafasi kubwa zaidi ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huu kutokana na mwenendo mzuri ambao imekuwa nao msimu huu, lakini pamoja na kuanza kufunga bado mambo yalikuwa magumu.

Staa Alexis Mac Allister alikuwa wa kwanza kufungia bao Liverpool katika dakika ya 14 tu ya mchezo lakini dakika chache mbele mambo yalibadilika.

Fulham ambayo ipo kwenye kiwango bora msimu huu ilifanikiwa kuongoza kwa mabao 3-1 hadi mapumziko baada ya kufunga bao la kuswazisha dakika ya 23 kupitia kwa Ryan Sessegnon, Alex Iwobi dakika ya 32 na Rodrigo Muniz dakika ya 37 ya mchezo.

Kipindi cha pili Liverpool ilirejea ikiwa na nguvu baada ya kutawala mchezo huo ikipoteza nafasi kadhaa za wazi lakini ikafanikiwa kufunga bao la pili kupitia kwa Luis Diaz katika dakika ya 72 ya mchezo huo.

Kutokana na kichapo hiki sasa Liverpool imeendelea kukaa kileleni ikiwa na pointi 72 zikiwa ni 11 mbele ya Arsenal inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo, huku Fulham ikisogea hadi nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa na pointi 48.

Mchezo mwingine uliushuhudia Chelsea ikishindwa kuchomoza na ushindi dhidi ya Brentford na mchezo kumalizika kwa suluhu.

Matokeo yanaweka rehani nafasi ya Chelsea ambayo ilikuwa nafasi ya nne na pointi 53 kabla ya mchezo wa kati ya Man City iliyopo nafasi ya tano na Man United.

Spurs ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Southampton kwa mabao yaliyofungwa na Brenan Johnson mawili na Mathes Tel, huku Saints wakifunga kupitia kwa Mateus Fernandez. Kwa matokeo haya Saints imeshuka daraja rasmi.