Ligi ya Mabingwa Ulaya imerejea na vita ya kuwania nafasi

Muktasari:
- Idadi ya michezo kwenye mfumo huu mpya umebadilika kutoka michezo 125 kwenye mfumo uliopita na kuwa 189.
Ligi ya Mabingwa Ulaya itaendelea kutimua vumbi leo Januari 21, 2025 baada ya kusimama tangu Desemba mwaka jana.
Mabingwa wa mwaka 2019 Liverpool watakuwa nyumbani kuikaribisha Lille ya Ufaransa. Liverpool inaongoza msimamo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 18 ambapo imeshinda mechi zote sita ilizocheza.
Mara ya mwisho Liverpool ilicheza Desemba 10, 2025 dhidi ya Girona ambapo alipata ushindi wa bao 1-0 wakati Lille nayo inaingia na kumbukumbu ya kushinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Sturm Graz.
Barcelona inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa na pointi 15 itakuwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya Benfica ya Ureno ambayo inashika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 10.
Juventus baada ya kushinda 2-0 dhidi Man City Desemba 11, 2025 itakuwa genini dhidi ya Club Brugge ambayo nayo mechi ya mwisho ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sporting.
Juventus inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 11 huku ikiitaji kuongeza pointi zitakazo ifanya imalize nafasi nane za juu wakati Club Brugge yenyewe inashika nafasi ya 19 pia ikiitaji kuongeza pointi ili kujinusuru kushuka nafasi za chini.
Diego Simeone ataiongoza Atletico Madrid kuivaa Bayern Leverkusen ya Xabi Alonso katika dimba la Riyadh Air Metropolitano nchini Hispania.
Atletico Madrid inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo ikiwa na pointi 12 huku Bayern Leverkusen inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 13. Katika mchezo wa leo vijana wa Simeone watahitaji pointi tatu ili kuipita Bayern Leverkusen.
Mchezaji anayeongoza kwa mabao hadi sasa ni Robert Lewandowski wa Barcelona mwenye mabao saba akifuatiwa na Jonathan David wa Lille na Juninho wa Qarabag FK wenye mabao sita.
Idadi ya michezo kwenye mfumo huu mpya umebadilika kutoka michezo 125 kwenye mfumo uliopita na kuwa 189.
Katika mfumo wa sasa timu 36 zitakuwa zikicheza mechi nane kwenye mfumo wa nyumbani na ugenini. Timu nane zitafuzu moja kwa moja kwenda hatua ya 16 Bora timu nyingine 24 zitacheza mtoano na nane zitakwenda hatua ya 16 Bora ambazo zitaingia robo fainali na nusu fainali, kabla ya mbili kucheza mchezo wa fainali.
Mechi za leo UEFA
AS Monaco vs Aston Villa FC
Atalanta vs Sturm Graz
Atlético Madrid vs Bayer Leverkusen
Bologna vs Borussia Dortmund
Club Brugge vs Juventus
Crvena Zvezda vs PSV Eindhoven
Liverpool FC vs LOSC Lille
Slovan Bratislava vs VfB Stuttgart
Benfica - FC Barcelona