Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe Neymar angetwaa Ballon d'or tatu

Muktasari:

  • Kiungo huyo raia wa Colombia ambaye kwa sasa anaitumikia Leon ya Mexico amesema kama si uwepo wa mastaa hao, basi Neymar angetwaa tuzo tatu za  Ballon d’Or.

Santos, Brazil. Staa wa zamani wa Real Madrid, James Rodriguez amesema kuwa mastaa wawili, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo walimzuia Neymar kutwaa  tuzo maarufu ya Ballon d'or.

Kiungo huyo raia wa Colombia ambaye kwa sasa anaitumikia Leon ya Mexico amesema kama si uwepo wa mastaa hao, basi Neymar angetwaa tuzo tatu za  Ballon d’Or.

Kiungo huyo mwenye miaka 33, sasa amesema anachokifanya staa wa Barcelona kwa sasa Lamine Yamal ndicho alichokuwa akifanya Neymar wakati wa ubora wake.

“Kwenye mawazo yangu, kama siyo uwepo wa Lionel Messi na Ronaldo wakati Neymar akiwa na ubora wa juu basi angeweza kutwaa  Ballon d’Or mara tatu, kuna vipindi unaona alishindwa kwa kuwa hawa walikuwepo.

"Lakini kupambana na hawa magwiji ni kazi kubwa sana, hawa walikuwa na ubora wa kipekee kwenye soka duniani na walistahili kila walichochukua," alisema mshambuliaji huyo.

Akizungumza kuhusu kiwango cha Madrid kwa sasa, Rodriguez amesema anaamini bado inaweza kufanya vizuri kwa kuwa imefanya usajili bora wa mshambuliaji Kylian Mbappe, ingawa amekuwa haangalii mechi zao mara kwa mara.

Neymar baada ya kusumbuliwa na majeraha kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita kwa sasa amerudi kwenye timu yake ya zamani ya Santos akiwa na kiwango bora zaidi uwanjani.

Mshambuliaji huyo ambaye ameachwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil ameshaichezea timu hiyo michezo saba, amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.

Hizi zinaonekana kuwa namba bora zaidi kwa mshambuliaji huyo kuliko miaka miwili ambayo amekaa kwenye kikosi cha Al Hilal cha Saudi Arabia ambapo alicheza michezo saba na kufunga bao moja tu.

Anatajwa kama mchezaji bora zaidi kwenye ligi hiyo ambaye amesajiliwa kwenye dirisha dogo la Januari 2025.

Takwimu zinaonyesha kuwa alifanikiwa zaidi wakati anaanza soka lake akiwa na Santos ambapo alicheza michezo 225 na kufunga mabao 136, ambapo aliondoka hapo na kujiunga na Barcelona ambapo napo alitumika kwenye michezo 186 na kupachika mabao 105, kabla hajaenda PSG ya Ufaransa alipotumika kwenye misimu sita, alicheza michezo 173 na kufunga mabao 118.