Kipengele cha Mchezaji Bora chateka tuzo za TFF leo

Muktasari:
- Msimu huu kutakuwa na ongezeko la tuzo tatu ambazo hazikuwepo msimu uliopita na kati ya hizo tuzo mbili ni mpya hazijawahi kutolewa, wakati tuzo moja iliwahi kutolewa lakini msimu uliopita haikuwepo.
Shirikisho la Soka Tanzania leo linatarajiwa kutoa tuzo za wachezaji waliofanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara, Ligi Kuu ya Wanawake pamoja na Kombe la Shirikisho la CRDB kwa msimu uliopita wa 2023/2024.
Tuzo hizo ambazo sherehe zake zitafanyika kwenye Ukumbi wa Warehouse Masaki leo jioni, zimegawanyika katika makundi matano ambayo ni, Tuzo za Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB, Tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake, Tuzo za Ligi Kuu ya NBC, Tuzo za Utawala, na Tuzo za ligi nyingine.
Hata hivyo, kipengele cha mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara ndiyo kinaonekana kuwa na vita kubwa ambapo watakuwa wakiwania wachezaji wanane ambao ni Stephen Aziz Ki (Yanga), Feisal Salum (Azam FC), Kipre Junior (Azam FC), Djigui Diarra (Yanga SC), Ley Matampi (Coastal Union), Kouassi Yao (Yanga SC), Mohamed Hussein (Simba SC) na Ibrahim Abdallah (Yanga SC).
Hata hivyo, mbali na vita ya mchezaji bora, kipengele kingine ambacho kinaonekana kusubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka leo ni kile cha beki bora ambacho kinawaniwa na Kouassi Yao (Yanga SC) Ibrahim Abdallah (Yanga SC) na Mohammed Hussein (Simba SC).
Msimu huu kutakuwa na ongezeko la tuzo tatu ambazo hazikuwepo msimu uliopita na kati ya hizo tuzo mbili ni mpya hazijawahi kutolewa, wakati tuzo moja iliwahi kutolewa lakini msimu uliopita haikuwepo.
Tuzo mpya ni Mchezaji Bora wa Tanzania anayecheza Nje (Mwanaume) na Mchezaji Bora wa Tanzania anayecheza Nje (Mwanamke).
Tuzo nyingine ni Mchezaji Bora wa Soka la Ufukweni.
Orodha kamili ya tuzo hizo na wateule wake ni kama ifuatavyo:
TUZO ZA KOMBE LA CRDB.
Mfungaji Bora
1:Clement Mzize – Yanga SC.
2: Edward Songo – JKT Tanzania.
KIPA BORA
1:Djigui Diarra – Yanga SC.
2:Khomeiny Abubakar – Singida Black Stars
3: Mohamed Mustapha – Azam FC
TUZO ZA LIGI KUU YA WANAWAKE
Mfungaji Bora
1:Aisha Mnuka – Simba Queens
Kipa Bora
1:Najath Abbas – JKT Queens
2:Caroline Rufaa – Simba Queens
3:Mariam Shaaban – Bunda Queens
Mchezaji Bora
1:Aisha Mnuka – Simba Queens
2:Stumai Abdallah – JKT Tanzania
3:Kaenda Wilson – Yanga Princess
4:Violeth Nichaus – Simba Queens
5:Vivian Corazone – Simba Queens
Kocha Bora
1:Juma Mgunda – Simba Queens
2:Esther Chabruma – JKT Queens
3:Noah Kanyoga – Ceasia Queens
Kikosi Bora kitatangazwa ukumbini
Mchezaji bora Chipukizi
1:Esther Maseke – Bunda Queens
2:Lydia Kabambo – JKT Queens
3:Bituro Mgosi – Bunda Queens
MWAMUZI MSAIDIZI BORA
1:Sikudhan Mkurugwa
2:Glory Tesha
3:Zawadi Yusuph
4:Monica Wazael
5:Getruda Getvas
Mwamuzi Bora
1:Amina Kyando
2:Tatu Malogo
3:Anitha Kisoma
4:Esther Adalbert
Timu yenye Nidhamu
1:Bunda Queens
2:Simba Queens
TUZO ZA LIGI KUU YA NBC (PL)
Mchezaji bora
1:Stephen Aziz Ki – Yanga SC
2:Feisal Salum – Azam FC
3:Kipre Junior – Azam FC
4:Djigui Diarra – Yanga SC
5:Ley Matampi – Coastal Union
6:Kouassi Yao – Yanga SC
7:Mohamed Hussein – Simba SC
8: Ibrahim Abdallah – Yanga SC
Kipa Bora
1:Ayoub Lakred – Simba SC
2:Djigui Diarra – Yanga SC
3:Ley Matampi – Coastal Union
Beki Bora
1:Kouassi Yao – Yanga SC
2:Ibrahim Abdallah – Yanga SC
3:Mohamed Hussein – Simba SC
Kiungo Bora
1:Stephen Aziz Ki – Yanga SC
2:Feisal Salum – Azam FC
3:Kipre Junior – Azam FC
Kocha Bora
1:David Ouma – Coastal Union.
2:Bruno Ferry – Azam FC.
3:Miguel Gamondi – Yanga SC.
Kikosi Bora Cha Msimu 2023/2024 kitatangazwa ukumbini
Meneja Bora
1:Amri Juma – Azam Complex
2:Nasser Makau – Mkwakwani
3:Shaaban Rajabu – Lake Tanganyika
Kamishina Bora
1:Martin Kibua – Tanga
2:Zena Chande – Dar Es Salaam
3:Hamis Kitila – Singida
4:Sadick Jumbe – Mbeya
5:Abousufian Silia – Iringa
Mchezaji bora Chipukizi
1:Semfuko Charles – Coastal Union
2:Shomary Raheem – KMC FC
3:Constantine – Malimi – Geita Gold.
Gold.