Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi kuimarisha ulinzi mechi ya Simba, Stellenbosch

POLISI Pict

Muktasari:

  • Mchezo huo utachezwa Jumapili Aprili 20, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia 10:00 jioni.

Zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba na Stellenbosch ya Afrika Kusini utakaopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex mjini Zanzibar, Jeshi la Polisi limeonya kuwa mashabiki wanapaswa kuzingatia taratibu zilizowekwa vinginevyo halitasita kuwachukulia hatua watakaozikiuka.

Jeshi hilo limesema ulinzi utaimarishwa kipindi chote cha kabla na baada ya mchezo ili kuwahakikishia usalama mashabiki watakaojitokeza.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Abubakar Khamis Ally amesema jeshi hilo linatambua mchezo huo ni mkubwa na umebeba taswira na heshima ya Tanzania hivyo watahakikisha usalama unaimarishwa katika maeneo ya ndani na nje ya uwanja.

"Hivyo hakutakuwa na nafasi wala muhali kwa mtu yeyote atakayefanya vitendo vyenye kuleta uvunjifu wa amani kwa namna yeyote... tutahakikisha kuwa wananchi, wanachama, mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu wanashiriki katika mchezo huo kwa usalama na amani," amesema Abubakar.

Amesema pamoja na kuwepo kwa mechi hiyo, pia siku hiyo waumini wa dini ya Kikristo watakuwa wanasherehekea Sikukuu ya Pasaka, mambo ambayo yanalisukuma jeshi hilo kuboresha zaidi ulinzi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama mjini humo.

Simba tayari imeshatua mjini Unguja kujiandaa na mchezo huo baada ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa kwa muda ili kupisha maboresho na ukarabati.