Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo FIFA kusimamia uchaguzi TFF, wajumbe vikao haviishi

Muktasari:

  • Nafasi saba zinawaniwa katika Uchaguzi Mkuu wa TFF unaofanyika Jumamosi, Agosti 16, 2025.

Tanga. Mjumbe wa Baraza la Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Souleyman Waberi ataongoza ujumbe wa Shirikisho hilo kushuhudia Uchaguzi Mkuu wa TFF utakaofanyika kesho Jumamosi, Agosti 16, 2025 jijini Tanga.

Waberi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Djibouti, ameingia Tanga leo jioni akiwa na maofisa wengine kadhaa wa shirikisho hilo na lile la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Mjumbe wa Baraza la Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Souleyman Waberi.

Ujumbe wa Waberi umefikia katika Hoteli ya Tanga Beach Resort ambako uchaguzi huo mkuu wa TFF utafanyika.

Idadi kubwa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ambao watashiriki Uchaguzi huo tayari imewasili jijini Tanga na wanaonekana kuwa tayari kwa zoezi hilo.

Furaha ya wajumbe wengi ilionekana mara baada ya taarifa ya kutupiliwa mbali kwa ombi la zuio la uchaguzi huo lililofunguliwa na Mawakili wanne katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam.

Wajumbe hao walionekana kukaa na kusimama vikundi vikundi wakijadili kuendelea kwa mchakato wa Uchaguzi huo huku baadhi ya wagombea na wapambe wao wakitumia fursa hiyo kuomba kura kwa wajumbe.

Usiku huu wajumbe na wageni mbalimbali wanashiriki hafla ya chakula cha jioni inayoendelea katika Hoteli ya Tanga Beach Resort.