Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kidao ajiengua TFF, tuzo Ligi Kuu zapelekwa Desemba

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidao

Muktasari:

  • Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ulifanyika Agosti 16, 2025 jijini Tanga.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidao ameamua kutoendelea na nafasi hiyo ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu lilipofanya Uchaguzi Mkuu.

Chanzo cha uhakika kutoka TFF kimefichua kwamba Kidao hatoongeza mkataba mpya baada ya ule wa mwanzo kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

“Mkataba wake utamalizika mwisho wa Septemba na ameamua kutoongeza hivyo shirikisho litakuwa na Katibu Mkuu mpya muda sio mrefu,” kimefichua chanzo hicho.

Kuondoka kwa Kidao kunahitimisha miaka nane ya utumishi wake katika nafasi hiyo aliyoitumikia tangu Agosti, 2017.

Kabla ya nafasi hiyo ya Ukatibu Mkuu, Kidao alihudumu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA).


Tuzo 2024/2024 Desemba

Wakati Kidao akijiweka kando, TFF imetangaza kuwa hafla ya tuzo za Shirikisho hilo kwa msimu wa 2024/2025 zitafanyika Desemba mwaka huu.

“Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwafahamisha wadau wa mpira wa miguu na umma kwa ujumla kuwa Hafla ya Tuzo (TFF Awards 2025) itafanyika mwanzoni mwa mwezi Desemba.

“Tarehe rasmi ya Hafla hiyo kwa ajili ya kutambua wanamichezo waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali kwa msimu wa 2024/2025 itatangazwa baada ya kukamilisha maandalizi mengine ikiwemo ukumbi.

“Katika hafla hiyo, zitatolewa tuzo katika makundi nane ya Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la benki ya CRDB, Ligi Kuu ya Wanawake, Ligi ya NBC ya Championship, First League, Ligi ya U20 ya NBC, na tuzo za Utawala.

Mchezaji Bora (MVP) kwa msimu wa 2024/2025 atafahamika usiku wa tuzo hizo ambazo huwakutanisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu ikiwemo Serikali pamoja na wadhamini,” imefafanua taarifa hiyo ya TFF.