Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ipswich ya Ed Sheeran yarudi Ligi Kuu England

Baadhi ya wachezaji wa Ipswitch wakishangilia moja ya bao katika mechi ya Championship dhidi ya Millwall iliyopigwa jana Mei 2, 2026. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Timu hiyo maarufu kama ‘The Tractor Boys’ wana kibarua kingine cha kuhakikisha wanabaki ndani ya Ligi Kuu, baada ya kurejea kwa kishindo.

Ipswitch, England. Klabu ya Ipswich Town imerejea rasmi katika Ligi Kuu England baada ya kupata ushindi hapo jana dhidi ya Millwall katika mchezo wa mwisho wa Championship.

Ushindi huo umeibua shamrashamra kubwa ndani na nje ya Uwanja wa Portman Road, huku wachezaji na benchi la ufundi wakisherehekea baada ya kuthibitisha kupanda daraja.

Kocha wa timu hiyo, Kieran McKenna, alibebwa juu na wachezaji wake ishara ya furaha ya kurejea Ligi Kuu ya EPL.

Mashabiki nao hawakuwa nyuma, wakivamia uwanja kusherehekea mafanikio hayo, huku msanii maarufu na mmoja wa wamiliki wa klabu hiyo, Ed Sheeran, akiungana nao kushangilia ushindi huo.

Katika mchezo huo, Ipswich ilianza kwa kasi na kujipatia mabao mawili ya haraka kupitia George Hirst na Jaden Philogene ndani ya dakika 10 za mwanzo.

Msanii maarufu na mmoja wa wamiliki wa klabu ya Ipswitch Town, Ed Sheeran wakati alipokuwa akishangilia pamoja na mashabiki wa timu hiyo baada ya kurejea Ligi Kuu England. Picha na Mtandao

Licha ya ugumu kutoka kwa wapinzani wao, bao la tatu lililofungwa na Kasey McAteer mwishoni mwa mchezo liliwahakikisha kukata tiketi ya kurejea tena Ligi Kuu.

Ipswich imefanikiwa kupanda daraja mara ya tatu ndani ya miaka minne, jambo linaloonyesha mabadiliko makubwa ndani ya klabu hiyo.

Kocha McKenna amekiri kuwa safari hiyo haikuwa rahisi, akieleza kuwa timu ililazimika kufanya kazi kwa bidii kurejea katika kiwango hicho baada ya kushuka daraja.

Awali, klabu hiyo ilikumbana na changamoto iliposhindwa kudumu kwenye Ligi Kuu, hali iliyochangiwa na kukosa uzoefu na nguvu ya kimwili ya kushindana katika kiwango hicho.

Baadhi ya mashabiki wa Ipswitch Town wakishangilia ndani ya uwanja wa Portman Road baada ya kurejea Ligi Kuu England. Picha na ,Mtandao

Hata hivyo, msimu huu Ipswich imeonekana kuwa na mbinu tofauti, ikicheza kwa nidhamu zaidi na kudhibiti michezo vizuri, jambo lililowasaidia kufikia mafanikio hayo.

Timu hiyo maarufu kama ‘The Tractor Boys’ wana kibarua kingine cha kuhakikisha wanabaki ndani ya Ligi Kuu, baada ya kurejea kwa kishindo.


Zitakazocheza mtoano

Timu nne zilizomaliza nafasi ya tatu hadi sita ambazo ni Millwall, Southampton, Middlesbrough na Hull City, zinakwenda kucheza mtoano 'play-offs' kuwania nafasi moja ya kupanda daraja ambapo zitaanzia nusu fainali, kisha fainali ambapo bingwa ndiye atapanda.


Zilizoshuka

Timu tatu zilizomaliza nafasi ya 22, 23 na 24 ambazo ni Oxford United, Leicester City na Sheffield Wednesday zimeshuka daraja ambapo msimu ujao zitashiriki League One.