Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyu hapa refa wa Simba, Berkane

Muktasari:

  • Aliwahi kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ambapo Wekundu wa Msimbazi walishinda mabao 2-0 dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco, Disemba 19, 2023.
yes

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limemteua mwamuzi wa kati, Pierre Ghislain Atcho kutoka Gabon kusimamia mechi ya kwanza ya fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya wenyeji, RS Berkane ya Morocco dhidi ya Simba kutoka Tanzania.

Atcho anakumbukwa zaidi na Simba, kwani aliwahi kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ambapo Wekundu wa Msimbazi walishinda mabao 2-0 dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco, Desemba 19, 2023.

Refa huyo atasaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja, Boris Marlaise Ditsoga wa Gabon, msaidizi namba mbili ni Eric Ayimavo Ayamr Ulrich wa Benin, huku refa wa akiba mezani atakuwa Patrice Tanguy Mebiame kutokea Gabon.’

Mwamuzi huyo aliyezaliwa Oktoba 10, 1992, rekodi zinaonyesha amechezesha mechi 24 za kimataifa, ambapo timu za nyumbani zimeshinda 12, za ugenini zimeshinda saba na tano zilizobakia zikiisha kwa sare, akitoa kadi za njano 101 na nyekundu moja.

Kwa upande wa Teknolojia ya Video Assistant Referee (VAR), katika mechi hiyo itaongozwa na Abongile Tom wa Afrika Kusini akishirikiana na Maria Packuita Cynquela Rivet wa Mauritania, huku msaidizi wa pili ni Diana Chikotesha kutokea Zambia.

Simba imetinga fainali baada ya kuitoa Stellenbosch ya Afrika Kusini katika hatua ya nusu fainali kwa kwa jumla ya bao 1-0 baada ya kucheza mechi mbili na sasa inakutana na RS Berkane ya Morocco iliyoitoa CS Costantine ya Algeria kwa jumla ya mabao 4-1.

Simba itaanza kampeni za kusaka taji hilo kwa kucheza fainali ya kwanza ugenini Mei 17 ikiwa Morocco, kisha baada ya hapo itarudi jijini Dar es Salaam kwa mechi ya marudiano itakayochezwa Mei 25, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa huku kombe likiwa Uwanjani.

Hii si mara ya kwanza kwa Simba SC kukutana na RS Berkane katika mashindano ya haya kwani Katika msimu wa 2021-2022 wa Kombe la Shirikisho Afrika, timu hizo zilikutana katika hatua ya makundi. Mechi ya kwanza ilichezwa Morocco ambapo RS Berkane ilishinda kwa mabao 2-0 na katika mechi ya marudiano iliyofanyika Dar es Salaam, Simba ilipata ushindi wa bao 1-0.

RS Berkane, inautafuta ubingwa huo kwa mara ya tatu baada ya kuchukua msimu wa 2019–2020, ilipoifunga Pyramids ya Misri bao 1-0 na msimu wa 2021–2022, ilitwaa ubungwa huo baada ya kuifunga Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa mikwaju ya penalti 5-4, baada ya sare ya 1-1.

Kwa upande wa Simba inasaka taji hilo kwa mara ya kwanza ikiwa inashiriki fainali ya michuano hii kwa mara ya kwanza. Fainali pekee ya Afrika ambayo Simba imewahi kucheza ni ya Kombe la CAF mwaka 1993, ambapo ilifungwa 2-0 na Stella Club d'Adjame ya Ivory Coast.