Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Havertz atupia Arsenal ikiukaribia ubingwa EPL

Muktasari:

  • Iwapo Arsenal wataibuka na ushindi dhidi ya Crystal Palace, watahakikisha wanatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 22.

London, England. Bao pekee alilofunga Kai Havertz limetosha kuipa pointi tatu muhimu Klabu ya Arsenal ambayo imebakiza mechi moja kumaliza msimu wa Ligi Kuu England wa 2025/2026.

Iwapo Washika Mitutu hao wa London watashinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Crystal Palace, Mei 24 mwaka huu, watakuwa ndio mabingwa wapya wa Ligi Kuu England kwani watafikisha jumla ya pointi 85 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote.

Katika mchezo wa jana uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirates, London, Arsenal ambao ndio walikuwa wenyeji walijihakikishia pointi tatu baada ya mshambuliaji wao Havertz kufunga bao la kichwa akimalizia krosi ya kona iliyopigwa na nahodha Bukayo Saka.

Mshambuliaji wa Arsenal, Kai Havertz wakati akifunga bao dhidi ya Burnley katika mechi ya Ligi Kuu England, Mei 18, 2026. Picha na Mtandao

Saka amefikisha idadi ya pasi za mabao 50 sawa na idadi ya mabao aliyofunga katika Ligi Kuu England akiwa na umri wa miaka 24 na siku 255 wakati mchezaji mwingine aliyewahi kufanya hivyo alikuwa ni Wayne Rooney alipokuwa na miaka 24 na siku 84.

Arsenal hadi sasa ndio vinara wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 82 wakifuatiwa na wapinzani wao wa karibu Man City wenye pointi 77 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Hata hivyo, Arsenal ‘The Gunners’ wanaweza kutangazwa kuwa mabingwa bila kusubiri mchezo wa mwisho iwapo ikitokea kama Man City watapoteza au kutoka sare katika mchezo wao dhidi ya Bournemouth.

Mshambuliaji wa Arsenal, Kai Havertz wakati akishangilia bao alilofunga katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Burnley, Mei 18, 2026. Picha na Mtandao


Shangwe zilivyotawala Emirates

Kulikuwa na shamrashamra kubwa kutoka kwa wachezaji pamoja na Meneja Mikel Arteta mara tu baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa, huku dalili za ubingwa wa Ligi Kuu zikizidi kuonekana.