Guirassy aomba kuondoka kisa Arsenal

Muktasari:

  • Msimu uliopita Guirassy alifunga mabao 28 katika mechi 28 alizocheza Bundesliga.

London, England. Staa anayesakwa na Arsenal, Serhou Guirassy amewaambia mabosi wa klabu yake ya Stuttgart kwamba anataka kuhama kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya, imeelezwa.

Straika huyo amekuwa moto kwelikweli tangu msimu uliopita baada ya kufunga mabao 28 katika mechi 28 alizocheza kwenye Bundesliga.

Jambo hilo limemfanya azivutie timu nyingi kubwa za Ulaya na huenda akashawishika na mpango wa kutua kwenye Ligi Kuu England.

Guirassy, 28, aliambia Stuttgart anataka kubadili timu kwenye dirisha hilo la majira ya kiangazi kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya usajili na uhamisho wa wachezaji, Florian Plettenberg.

Ripoti zinadai kwamba Arsenal ipo kwenye mbio za kunasa saini ya supastaa ahuyo wa kimataifa wa Guinea.

Lakini, kwenye kunasa saini yake Arsenal inakabiliwa na vita kali mbele ya Borussia Dortmund na AC Milan zinazohitaji huduma yake.

Newcastle United na Manchester United nazo kuna nyakati zilihusishwa na Guirassy hasa kwenye kipindi cha usajili wa Januari.

Kwa mujibu wa SunSport straika huyo huko nyuma aliwahi kutaka kwenda kujiunga na Tottenham Hotspur. Ukimweka kando staa huyo, Arsenal inahitaji pia huduma ya staa wa Hispania, Mikel Merino. Staa huyo wa zamani wa Newcastle alitumikia miezi sita iliyopita kwenye kikosi cha Real Sociedad, akiisaidia timu hiyo kushika nafasi sa juu kwenye msimamo wa LaLiga.

Ripoti hizo zilidai kwamba Chelsea ipo kwenye mazungumzo na mawakala wa Jonathan David, wakati Newcastle ikidaiwa kujitoa kwenye mbio za kunasa saini ya mshambuliaji wa Everton, Dominic Calvert-Lewin.


Dondoo zake

STUTTGART 2023-24
-Amecheza: Mechi 28
-Ametengeneza: Nafasi 53
-Amefunga: Mabao 28
-Ametoa: Asisti 2
-Amelenga lango: Mashuti 45
-Amepiga: Pasi 769