Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Galatasaray wakoleza tetesi kumsajili Messi

Muktasari:

  • Msimu uliopita, Galatasary ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uturuki na pia ilitwaa Kombe la Uturuki.

Rais wa Galatasaray, Dursun Ozbek ametoa majibu ya kijasiri baada ya kuulizwa iwapo miamba hiyo ya Uturuki itamsajili Lionel Messi.

Kumekuwepo na tetesi kwamba Galatasaray inataka kumsajili Messi kwa mkopo kuanzia Januari hadi Machi mwakani wakati Ligi Kuu Marekani (MLS) itakapokuwa imesimama.

Ozbek amesema kuwa timu yake inaweza kumsajili Messi au mchezaji mwingine yeyote yule kwani iko imara kiuchumi.

"Ulisema Messi? Hatua yenye mafanikio makubwa ya Galatasaray ni uhamisho iliofanya. Hatukufanya uhamisho mwingi, lakini tulifanya uhamisho tuliohitaji, tuliibakiza timu. Tuliweka uti wa mgongo wa timu ambayo imekuwa bingwa miaka mitatu mfululizo, hasa timu nzima.

"Naamini tulijenga timu yenye mafanikio kwa uhamisho. Tumepandisha daraja la juu sana. Tulifanya uhamisho wa juu kabisa wa soka la Uturuki katika ngazi ya juu kabisa ya soka la Uturuki.

"Tumeinua kiwango cha mafanikio kwa kiwango cha juu, kwa hivyo unaweza kuuliza swali la Messi kwa urahisi. Wakati tunafanya haya yote, tumefikia hali nzuri ya kifedha na hatufanyi chochote kitakachovuruga hii. Kazi zote tunazofanya, zlazima zibaki ndani ya uwezo wetu wa kifedha. Ndio maana tumeunda timu nzuri na tunatumai kuwa tuna malengo Ulaya. Tutafanya chochote kinachohitajika kufikia malengo haya," ametamba Ozbek.

Galatasaray wameshinda Ligi Kuu ya Uturuki katika misimu mitatu mfululizo iliyopita. Walivuna rekodi ya pointi 102 msimu wa 2023-24 na pia walishinda Kombe la Uturuki msimu uliopita.

Klabu hiyo yenye maskani yake Istanbul imefanya usajili mkubwa katika misimu michache iliyopita. Walisajili wachezaji kama Mauro Icardi, Wilfried Zaha, Lucas Torreira na Dries Mertens na pia kuvunja rekodi ya uhamisho ya Uturuki kwa kumsajili Victor Osimhen kwa Pauni 65 milioni