Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fadlu acheza na akili za Waarabu

Fadlu Pict

Muktasari:

  • Simba inaenda kukutana na wapinzani hao katika mchezo utakaopigwa Jumapili ya Januari 5, 2025, kwenye Uwanja wa Hammadi Agrebi uliopo Jiji la Tunis, huku ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-1, mechi ya kwanza Dar es Salaam, Desemba 15, 2024.

Kikosi cha Simba, kinatarajia kuondoka nchini kesho Jumatano alfajiri kwenda Tunisia kwa ajili ya mchezo wa nne wa makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien ya nchini humo, huku kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids akicheza akili kubwa.

Simba inaenda kukutana na wapinzani hao katika mchezo utakaopigwa Jumapili ya Januari 5, 2025, kwenye Uwanja wa Hammadi Agrebi uliopo Jiji la Tunis, huku ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-1, mechi ya kwanza Dar es Salaam, Desemba 15, 2024.

Moja ya jambo ambalo Fadlu ameliwekea msisitizo ni kutotaka kuwapa mapumziko marefu wachezaji wake tangu mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara walioibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Singida Black Stars, Uwanja wa Liti, Desemba 28 mwaka huu.

Bao la timu hiyo lilifungwa na Mkongomani, Fabrice Ngoma na kukifanya kikosi hicho kushinda michezo tisa mfululizo ya Ligi Kuu Bara tangu mara ya mwisho ilipochapwa bao 1-0 na watani zao, Yanga Oktoba 19 mwaka huu.

Kutokana na ushindi huo, uongozi ulipanga kutoa mapumziko ya siku tatu hadi nne ingawa Fadlu alibadili gia angani na kutaka mastaa wote kuwasili kambini mapema, ili kupata muda mrefu wa kufanya mazoezi wakiwa Tunisia unapochezwa mchezo huo.

“Tulihitaji kupata muda mrefu wa kufanya mazoezi kwa takribani siku tatu hadi nne tukiwa Tunisia kwa ajili ya kuzoea mazingira, tuliona kipindi hiki tuna michezo migumu iliyokuwa mbeleni, hivyo tusingependa kupoteza malengo tuliyonayo,” alisema Fadlu.

Fadlu alisema anatambua wachezaji wako katika wakati ambao kila mmoja anawaza sikukuu za mwisho wa mwaka ingawa isingekuwa jambo nzuri kuwapa muda mrefu wa kufurahia na familia zao, kutokana na umuhimu wa michezo ijayo.

“Kwa sasa malengo yetu ni Tunisia lakini baada ya hapo tuna safari nyingine ya Angola kucheza na Bravos do Maquis, sasa utaona ni jinsi gani tunapaswa kuendeleza kile tulichokifanya katika Ligi Kuu ili tusitoke nje ya mstari wetu,” alisema.

Simba iliyocheza michezo mitatu ya Kundi A na kushinda miwili huku ikipoteza mmoja na kukusanya pointi sita, inaenda kukutana na CS Sfaxien inayoburuza mkiani kutokana na kutoshinda mechi yeyote, kisha kuifuata Bravos Januari 12, 2025.

Simba haitakuwa na presha kubwa ya wapinzani hao hasa baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuishushia rungu SC Sfaxien kwa kuitoza faini ya Dola 50,000 sawa na Sh119 milioni na kuzuia mashabiki kuingia uwanjani katika michezo yao miwili ya nyumbani.

Hatua hiyo ilijiri baada ya CAF kuitia hatiani CS Sfaxien kutokana na vurugu za mashabiki wa kikosi hicho katika mchezo wa kwanza wa makundi Kombe la Shirikisho Afrika, ilipochapwa nyumbani bao 1-0 dhidi ya CS Constantine ya Algeria Novemba 27, 2024.

Baada ya mchezo huo kwa Simba na Watunisia, hesabu za kikosi hicho cha ‘Wekundu wa Msimbazi’ zitaelekea Angola kucheza dhidi ya Bravos Januari 12, huku ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi ya kwanza bao 1-0 nyumbani, la Jean Charles Ahoua Novemba 27 mwaka huu. Itamaliza nyumbani kukabiliana na CS Constantine Januari 19, 2025.