Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick na mtihani mgumu Man United leo

Muktasari:

  • Kwa sasa, United iko katika nafasi nzuri ya kumaliza ndani ya tano bora, huku ikihitaji ushindi dhidi ya Brentford ili kuendelea kujichimbia katika nafasi za juu.

Manchester, England. Kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick anatajwa kuwa katika mtihani mgumu utakaoamua mustakabali wake ndani ya Old Trafford wakati timu hiyo ikishuka dimbani dhidi ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Mchezo huo unatajwa kuwa na uzito mkubwa kwa Carrick, kwani ushindi unaweza kuipeleka United katika nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao jambo ambalo linaweza kumshawishi mmiliki mwenza wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe, kumpa kibarua cha kudumu.

Carrick, aliyechukua mikoba ya ukocha Januari mwaka huu baada ya kuondoka kwa Ruben Amorim, ameweka wazi kuwa lengo lake kuu ni kuirejesha United kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Kwa sasa, United iko katika nafasi nzuri ya kumaliza ndani ya tano bora, huku ikihitaji ushindi dhidi ya Brentford ili kuendelea kujichimbia katika nafasi za juu.

Akizungumza, Carrick amesema kushiriki Ligi ya Mabingwa ni ndoto ya klabu hiyo na mashabiki wake.

“Ligi ya Mabingwa ndiyo mahali tunapotaka kuwa. Hatuwezi kuchukulia kirahisi, lakini tupo kwenye nafasi nzuri na tunahitaji kumalizia kazi,” amesema Carrick.

Mbali na matokeo ya uwanjani, Carrick pia anaungwa mkono ndani ya United, jambo linalomfanya aonekane kuwa chaguo sahihi kwa muda mrefu licha ya kutokuwa na haiba ya ukali inayodaiwa kupendwa na Ratcliffe kwa makocha.

Inadaiwa kuwa wawili hao walikutana hivi karibuni katika mazungumzo yasiyo rasmi, hatua inayotafsiriwa kama sehemu ya tathmini ya uongozi wa klabu juu ya mustakabali wa benchi la ufundi.

Katika mchezo wa leo, United inatarajia kupata huduma ya beki Harry Maguire aliyemaliza adhabu yake, huku Lisandro Martinez akiendelea kutumikia adhabu baada ya rufaa yake kukataliwa.

Carrick ameonyesha kutoridhishwa na maamuzi ya waamuzi kuhusu adhabu hiyo, akidai hayakuwa ya haki ukilinganisha na matukio mengine yaliyotokea viwanjani.

Kwa ujumla, mchezo wa leo si wa kawaida kwa United, bali ni kipimo muhimu kwa Carrick kuthibitisha uwezo wake na kujiwekea mazingira mazuri ya kupewa nafasi ya kudumu ndani ya klabu hiyo kongwe ya England.