Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF kumalizana mapema na Yanga, Simba mtegoni

Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakishangilia moja ya bao katika ushindi wa 3-0 waliopata katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union. Picha na Yanga

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na pointi 54 ilizokusanya katika mechi 22.

Dar es Salaam. Yanga inaufuata kwa kasi ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu ambapo kama itapata ushindi katika mechi saba kati ya nane zilizobakia, itajihakikishia taji pasipo kutegemea matokeo ya timu nyingine.

Ikiwa itashinda mechi saba zijazo, itafikisha pointi 75 ambazo hakuna timu nyingine yoyote inayoweza kuzifikia na hivyo itatetea taji hilo.

Wakati ikijiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa taji la Ligi Kuu, Yanga na nafasi kubwa ya kuwa timu ya kwanza kuzikaribia noti za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Noti hizo ni zile zitokanazo na ushiriki katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kila timu inayokuwa na tiketi ya kucheza mashindano hayo, inajihakikishia kuvuna kitita cha Dola 100,000 (Sh260 milioni).

Tofauti na ubingwa ambapo inahitajika kupata ushindi katika mechi saba kati ya nane ilizobakiza, katika kusaka tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inatakiwa kupata ushindi katika mechi tano tu kati ya nane ilizobaki nazo ili iwe na uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao pasipo kutegemea matokeo ya timu nyingine.

Ushindi kwa Yanga katika mechi hizo tano, utaifanya ifikishe pointi 69 ambayo itaihakikishia kumaliza katika nafasi mbili za juu ambazo ndio za uwakilishi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mambo yanaweza kuwa rahisi zaidi kwa Yanga na ikajikuta ikihitajika kupata ushindi katika mechi chache badala ya tano, ikiwa Simba na Azam zitaangusha pointi njiani.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa Yanga, Simba inahitajika kupata ushindi katika mechi sita na kutoka sare moja katika mechi nane ilizobakiza iili ijihakikishie kuwemo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ugumu wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika unaonekana kuwepo zaidi kwa Azam FC ambayo kwanza inatakiwa kupata ushindi katika mechi zake zote nane zilizosalia na pili kuziombea Yanga na Simba ziangushe pointi kwenye baadhi ya michezo.

Simba ina pointi 49 huku Azam ikiwa na pointi 43. Kwa upande mwingine, Yanga inahitajika kupata ushindi katika mechi mbili tu zinazofuata ili ijihakikishie rasmi kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao mojawapo kati ya Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho Afrika.

Ikishinda mechi mbili zijazo, Yanga itafikisha pointi 60 ambazo zitaihakikishia kumaliza katika nafasi tatu za juu ambazo zote zinatoa uwakilishi kimataifa.

Wakati miamba hiyo mitatu ikipambania tiketi mbili za kuiwakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, kwingineko Afrika, idadi ya timu 23 zimeshajihakikishia kucheza mashindano hayo msimu ujao.

Timu hizo ni Orlando Oirates na Kaizer Chips (Afrika Kusini), Rangers na Rivers United (Nigeria), MC Alger (Algeria), Aigle Noir (Burundi), Power Dynamos (Zambia), Rahimo (Burkina Faso), Foullah Edifice (Chad), Horoya (Guinea), ASEC Mimosas (Ivory Coast) na Mighty Wanderers (Namibia).

Nyingine ni UD Songo (Msumbiji), FC Nouadhibou (Mauritania), El Merrikh Bentiu (Sudan Kusini), La Cure Waves (Mauritius), Gaborone United (Botswana), Club Africain (Tunisia), African Stars (Namibia) na Lijabatho (Lesotho).