Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi 'mtarajiwa' Arsenal wasifu umenyooka

Muktasari:

  • Atletico Madrid inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania ikiwa na pointi 56 wakati huo Arsenal ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) ikiwa na pointi 54.

Mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Atletico Madrid, Andrea Berta (53) anatajwa kuchukua nafasi ya mkurugenzi wa michezo wa Arsenal ya England.

Nafasi hiyo iko wazi ndani ya klabu ya Arsenal tangu Novemba mwaka jana kufuatia kuondoka ghafla kwa Edu Gaspar.

Inaripotiwa kwamba hadi sasa, Berta ndio anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo mbele ya kundi kubwa la waliotuma maombi wakiwemo nyota wawili wa zamani wa Arsenal, Tomas Rosicky na Gilbetob Silva.


Uzoefu wa kutosha

Kabla ya kuingia kwenye soka, Berta ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara alikuwa akifanya kazi benki kwa muda wa miaka 30.

Maisha ya soka alianza kujihusisha nayo mwaka 2002 akianzia katika timu ya AC Carpenedolo ambayo ilikuwa inashiriki Ligi Daraja la t`atu Italia aliyoitumikia hadi 2006 na kazi nzuri aliyoifanya hapo iliishawishi Parma kumchukua na kumpa kazi ya mkurugenzi wa michezo.

Alidumu Parma hadi 2009 ambapo aliachana na timu hiyo na kujiunga na Genoa ambako aliendelea na jukumu lilelile alilokuwa nalo Parma la mkurugenzi wa michezo na Mei 2013 akatimkia Atletico Madrid ambako alianzia na jukumu la mkurugenzi wa ufundi.

Kazi nzuri aliyoifanya katika kusimamia idara ya ufundi kwenye timu hiyo. iliishawishi Atletico Madrid kumpandisha cheo na kumpa nafasi ya mkurugenzi wa michezo, ambayo ameitumikia kwa zaidi ya miaka minne kuanzia Julai 2017 alipopandishwa hadi Januari mwaka huu alipoamua kuachana nayo.


Sajili za kibabe

Heshima kubwa ambayo Berta ameipata ndani ya Atletico Madrid ni usajili wa wachezaji wazuri ambao wamekuwa chachu ya mafanikio ambayo klabu hiyo imekuwa ikiyapata katika miaka ya hivi karibuni.

Mfano wa nyota ambao Berta amefanikisha kupatikana kwao na kujiunga na Atletico Madrid ni Jan Oblak, Antoine Griezmann, Rodri na Yannick Carrasco.

Na Berta ndiye amefanya sajili za Julian Alvarez, Alexander Sorloth na Conor Gallagher ambao wameonekana kuwa wachezaji muhimu katika ujenzi wa kizazi kipya cha timu hiyo.


Upepo wa mataji

Katika kipindi cha miaka 11 aliyoitumikia Atletico Madrid, timu hiyo imefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya Hispania, taji moja la Europa League, taji moja la Copa Del Ray, kombe la Hispania na taji moja la Super Cup Ulaya.

Mwaka 2019, Muitaliano huyo alifanikiwa kupata tuzo ya mkurugenzi bora wa michezo wa mwaka iliyotolewa na Globe Soccer Awards.