Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao la Mayele laiibua Yanga, Pyramids, AS Vita nazo zampa tano

Muktasari:

  • DR Congo ilianza fainali hizo kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Ureno na mchezo uliofuata ikapoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Colombia kisha ikaifunga Uzbekistan kwa mabao 3-1.

Yanga imempongeza mshambuliaji wa DR Congo, Fiston Mayele kwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 ambao timu yake imeupata dhidi ya Uzbekistan Alfajiri ya kuamkia leo.

Ushindi huo umeifanya DR Congo kumaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi K na kutinga katika hatua ya 32 Bora.

DR Congo imefuzu katika hatua hiyo ikibebwa na kigezo cha kuwa miongoni mwa timu nane zilishika nafasi ya tatu zikiwa na matokeo bora katika hatua ya makundi (Best Losers). Yanga imeandika kwamba kwa kufanya hivyo, Mayele ameandika historia.

"Hongera Fiston Mayele kwa kufunga bao lake la kwanza kwenye Fainali za Kombe la Dunia. Ameandika historia.

kwa kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kucheza klabu yetu na Ligi Kuu Tanzania kufunga katika Fainali za Kombe la Dunia," imesema Yanga.

Mbali na Yanga, Pyramids FC anayoichezea sasa hivi na AS Vita Club aliyowahi kuichezea zamani nazo zimempongeza Mayele.

Klabu yake ya zamani, AS Vita imeonyeshwa kufurahishwa na bao hilo na imesema kuwa mshambuliaji huyo amekuwa akifanya mambo makubwa katika mechi muhimu.

"Cyborg Kwa wengine inawe-za kuwa jambo la ghafla laki-ni kwa AS Vita Club, ni tabia

yake kufunga katika nyakati za uamuzi," iliandika AS Vita Club.

Kabu yake ya sasa, Pyramids

FC imeandika, "Mayele ameweka historia. Goli la uamuzi lililochangia DR Congo kufuzu hatua ya mtoano. Kwa mara ya kwanza katika historia."

DR Congo ilianza fainali hizo kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Ureno na mchezo uliofuata ikapoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Colombia.

Katika mchezo huo, Mayele alifunga bao katika dakika ya 78 akimalizia pasi ya Meschack Elia.

Mayele aliingia uwanjani katika dakika ya 51 kuchukua nafasi ya Cedric Bakambu.