Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aston Villa, Crystal Palace zafuata nyayo za Arsenal na rekodi Ulaya

Muktasari:

  • Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itafanyika Mei 30, ya Europa League itachezwa Mei 20 na ile ya Conference League itakuwa Mei 27.

Historia mpya imeandikwa katika Ligi Kuu England (EPL) baada ya timu zake tatu kufuzu hatua ya fainali katika mashindano tofauti Ulaya msimu huu.

Hiyo inafuatia ushindi ambao Aston Villa imeupata jana usiku dhidi ya Nottingham Forest kwenye Europa League na ule ambao Crystal Palace imeupata mbele ya Shakhtar Donetsk katika Conference League.

Kocha wa Arsenal, Mike Arteta akishangilia na wachezaji wake baada ya timu hiyo kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Timu hizo zinafuata nyayo za Arsenal ambayo Jumanne iliyopita ilitinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuitupa nje Atletico Madrid.

Katika mechi za jana, Aston Villa imeibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Nottingham Forest na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1.

Nahodha wa Aston Villa, John McGinn akishangilia moja ya bao alilofunga katika mchezo wa nusu fainali ya Europa Dhidi ya Nothingham Forest.

Katika mchezo wa jana, mabao ya Aston Villa yamepachikwa na John McGinn aliyepachika mawili huku Ollie Watkins na Emiliano Buendia kila mmoja akipachika bao moja.

Aston Villa katika mechi ya fainali itakutana na Freiburg ya Ujerumani ambayo imeitoa Braga ya Ureno.

Katika Conference League, Crystal Palace imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-2 dhidi ya Shakhtar Donetsk.

Mabao ya Crystal Palace jana yamefungwa na Ismaila Sarr na lingine la kujifunga la Pedro Henrique huku lile la Shakhtar likifungwa na Eguinaldo.