Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta awaonya mastaa Arsenal

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, akishangilia baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Tottenham katika mechi ya Ligi Kuu England. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Arsenal inatarajiwa kurejea uwanjani kesho Jumanne, itakapokwenda Ureno kucheza dhidi ya Sporting Lisbon katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

London, England. Baada ya Arsenal kuondoshwa kwenye Kombe la FA, kocha wa timu hiyo, Mikel Arteta, amewaambia wachezaji wa kikosi hicho lazima wajifunze na kukabiliana na vipindi vigumu kuendana na hali ngumu, vinginevyo watajikuta wakimaliza msimu bila taji.

Ndoto ya Arsenal kutwaa mataji matatu ilizimika juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa St Mary's baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Southampton katika robo fainali ya Kombe la FA.

Ross Stewart aliifungia Southampton bao la kuongoza dakika ya 35, kabla ya Viktor Gyokeres kuisawazishia Arsenal dakika ya 68 baada ya kuingia akitokea benchi. Hata hivyo, Arsenal ilishindwa kushikilia bomba na kuruhusu bao lingine dakika ya 85 kupitia Shea Charles.

Kwa matokeo hayo, Southampton imefuzu kwenda nusu fainali wakati Arsenal ikipata kipigo chao cha pili mfululizo baada ya awali kufungwa na Manchester City kwenye fainali ya Kombe la Carabao, kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Arteta alilazimika kupanga kikosi chenye wachezaji wapya kwa kiasi kikubwa kutokana idadi kubwa ya mastaa wake ambao ni majeruhi.

Mambo yalionekana kuwa magumu kwake baada ya Gabriel Magalhaes kuumia kipindi cha pili, huku Arteta akisema moja ya sababu zilizochangia kupoteza kwao ni hali mbaya ya hewa iliyokuwa ni upepo mkali pamoja na majeruhi.

"Lazima uendane na hali halisi na ukabiliane nayo. Ni lazima ujifunze kukabiliana na mazingira magumu katika mpira wa miguu ili kushinda taji, tunapaswa kuonyesha sisi ni nani. Tulikuwa na umiliki mkubwa wa mpira karibu na eneo la hatari. Tuliruhusu bao la kwanza kwa namna isiyo ya kawaida kwetu. Tulipata nafasi mbili kubwa ambazo tulipaswa kuzitumia. Ukifanya makosa ya kujilinda kama tulivyofanya, ni vigumu kufika nusu fainali," alisema Arteta.

Arsenal inatarajiwa kurejea uwanjani kesho Jumanne, itakapokwenda Ureno kucheza dhidi ya Sporting Lisbon katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.