Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta alalama Arsenal kutosajili

Muktasari:

  • Arsenal inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) ikwia imekusanya pointi 50 ilizokusanya katika michezo 24

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta amesikitishwa na timu yake kupita katika dirisha dogo la usajili la Januari 2025 bila kusajili mchezaji yeyote.

Kuumia kwa Gabriel Jesus na Bukayo Saka kulitegemewa kungeifanya Arsenal isajili katika dirisha la majira ya baridi lakini hilo halikutokea jambo ambalo Arteta alisema hajafurahishwa nalo.

"Tulikuwa na nia ya wazi ambayo ni siku zote dirisha linapofunguliwa, kusaka fursa za kuimarisha kikosi chetu kwa wachezaji ambao wanaweza kutipatia matokeo.

"Kwa wachezaji walio majeruhi, tumeathirika na hatujafanikiwa. Tumesikitishwa katika namna hiyo lakini pia tulikuwa makini sana kwamba tunahitaji kuleta aina fulani  ya wachezaji na tulipaswa kuwa na nidhamu ya hilo pia. Nadhani ndivyo tulivyokuwa.

"Ni katika wasifu, mchezaji ambaye tunaamini anaweza kutuweka bora zaidi. Kiuchumi kuna njia nyingi, mambo mengi ambayo tunapaswa kukaa nayo kwenye mstari ambao umetufanya tuwe hapa na kuanzia hapo kujaribu kuimarika," alisema Arteta.

Katika dirisha hilo dogo la usajili la Januari, wachezaji watatu waliondoka Arsenal ingawa wote walikuwa hawapo katika mipango ya Arteta kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Arsenal ilimpoteza beki wa kati Ayden Heaven (17) aliyetimkia Manchester United na mwingine ni Josh Robinson (20) aliyejiunga na Wigan Athletic mtawalia.

Mchezaji mwingine ambaye Arsenal ilimfungulia milango katika dirisha dogo la usajili ni Marquinhos ambaye alijiunga na Cruzeiro ya Brazil.

Katika dirisha hilo dogo, Arsenal ilitajwa kuwania saini ya mshambuliaji wa Astin Villa, Ollie Watkins lakini dau ala Pauni 40 milioni ambalo ilitoa, lilikataliwa ambapo ilitajiwa dau la Pauni 60 milioni ililoligomea.