Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yahamishia majeshi kwa Sesko

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig, Marcel Schafer na mwenzake wa Arsenal, Andrea Berta inaripotiwa kwamba kikao chao kimezungumzia gharama zote za uhamisho wa Sesko.

Leipzig, Ujerumani. Arsenal na RB Leipzig zimeanza mazungumzo kwa ajili ya uwezekano wa uhamisho wa mshambuliaji Benjamin Sesko katika dirisha kubwa la usajili mwezi huu.

Mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig, Marcel Schafer na mwenzake wa Arsenal, Andrea Berta inaripotiwa kwamba kikao chao kimezungumzia gharama zote za uhamisho wa Sesko.

Sesko ambaye ana umri wa miaka 21, amewekwa sokoni na RB Leipzig ambayo inahitaji kitita cha Pauni 75 milioni ili imruhusu nyota huyo raia wa Slovenia kuondoka klabuni hapo.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta hivi karibuni alikiri kwamba klabu hiyo inaweza kuvunja rekodi yake ya uhamisho katika jitihada za kuimarisha safu yao ta ushambuliaji katika dirisha la sasa la usajili la majira ya kiangazi.

"Bajeti ni kama wakati unafunga ndoa yako, unapanga harusi yako na mke wako na unampa bajeti na sio kidogo, huwa zaidi.

'Unapojenga nyumba, daima ni zaidi. Kwa kawaida hii hutokea. Unajiandaa kwa matukio tofauti. Kisha mambo ya bahati mbaya hutokea.Kuna vigezo vingi ambavyo vinaweza kutokea lakini kuna bajeti. Siku zote kuna wazo la kile tunachoweza kufanya, kile tunaweza kuboresha, vipaumbele vipi vitatimia na kisha tuone kama tunaweza kukifanya," alisema Arteta.

Arsenal pia wamezungumza na Sporting Lisbon kuhusiana na uwezekano wa kumnunua mshambuliaji Viktor Gyokeres.

Wakati huohuo kwa upande wa wanaoondoka, winga wa Arsenal Marquinhos amejiunga na Cruzeiro.

Mbrazil huyo alijiunga na Arsenal mnamo 2022 lakini alicheza mara moja tu kabla ya kutolewa kwa mkopo.

Arsenal inaonekana kuvalia njuga usajili wa mchezaji wa nafasi ya mshambuliaji wa kati jambo ambalo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na ufanisi duni ambayo imekua nayo katika msimu uliopita.

Katika mechi 38 za Ligi Kuu England msimu wa 2024/2025, Arsenal ilifunga mabao 69 yakiwa ni 22 pungufu ya mabao iliyopachika katika msimu wa 2023/2024 ambao ilimaliza ikiwa imepachika mabao 91.

Sesko anaonekana anaweza kuwa mtu sahihi wa kutatua tatizo hilo la Arsenal kutokana na uwezo wake wa kufumania nyavu na kupiga pasi za mwisho.

Nyota huyo wa Slovenia, katika Ligi Kuu Ujerumani 'Bundesliga' msimu uliomalizika, alihusika na mabao 18 katika mechi 33 za RB Leipzig ambapo alipachika mabao 13 na kupiga pasi tano zilizozaa mabao.