Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yachapwa nyumbani ikiweka rehani ubingwa EPL

Muktasari:

  • Arsenal haijapata ushindi wala sare katika mechi tatu mfululizo za mashindano ya ndani nchini England.

Arsenal imepoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth leo katika mechi ya nyumbani kwenye Uwanja wa Emirates, matokeo yanayozidi kufifisha ndoto yake ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL) msimu huu.

Ikitegemewa kuendeleza matokeo mazuri baada ya kupata ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ugenini dhidi ya Sporting Lisbon, Jumanne iliyopita, Arsenal imekutana na mshtuko wa kichapo hicho cha Bournemouth kinachowafanya wabakie na pointi zao 70 katika mechi 32 walizocheza.

Mabao ya Bournemouth yaliyoizamisha Arsenal katika mechi ya leo yamefungwa na Junior Kroupi na Alex Scott.

Aliyefunga bao pekee la Arsenal katika mchezo huo ni Viktor Gyokeres lakini halikutosha kuinusuru timu yake na kipigo.

Ni mechi ya tatu mfululizo kwa Arsenal kupoteza katika mashindano ya ndani England baada ya kufungwa na Man City mabao 2-0 katika fainali ya Carabao na kisha kufungwa mabao 2-1 na Southampton katika robo fainali ya Kombe la FA.

Ni matokeo ambayo hapana shaka yanafurahiwa na Manchester City kwani sasa ina nafasi ya kupunguza pengo la pointi baina yake na Arsenal kubakia tatu ikiwa itapata ushindi katika mechi mbili ilizonazo mkononi.

Manchester City kesho Jumapili, itakuwa ugenini Stamford Bridge kukabiliana na Chelsea.

Nyota wa zamani wa Arsenal, Martin Keown anaamini kilichoiangusha timu yake ni presha ya taji.

“Hii ni huzuni kubwa. Bournemouth walikuwa wa kipekee, lakini mara ngapi tunasema sasa? Unatakiwa kuwa bora zaidi ya walivyokuwa (Arsenal) leo.

“Presha leo ilikuwa kubwa sana na tulikosa nishati,” amesema Keown.

Arsenal sasa inakabiliwa na mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon, keshokutwa Jumatano, Aprili 15, 2026.

Katika mchezo wa kwanza ugenini huko Ureno, Arsenal ilipata ushindi wa bao 1-0.